Mahakama Kuu, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imeweka zuio la wabunge viti maalumu 19 waliovuliwa uanachama wa Chadema, kuondolewa bungeni, hadi uamuzi wa kesi ya madai Na. 16/2022, waliyofungua itakapotolewa uamuzi.
Zuio hilo limewekwa leo Jumatatu na Jaji John Mgetta, akitoa uamuzi wa maombi yaliyowewasilishwa mahakamani hapo na wabunge hao wakiongozwa na Halima Mdee, ya kuona mahakama hiyo iweke zuio la wao kuondolewa bungeni.
Ombi hilo limewasilishwa leo Jumatatu, wakati kesi ya madai ya msingi ilipokwenda kutajwa mahakamani hapo mbele ya Jaji John Mgetta.
Katika ombi hilo, mawakili wa wabunge hao Ikupilika Panya, Edson Kilatu na Mwamanenge, waliiomba mahakama iwekeze zuio hilo hadi kesi ya msingi itakaposikilizwa.
Mawakili wa wabunge hao, waliwasilisha maombi hayo wakidai uamuzi wa Baraza Kuu la Chadema, kutupilia mbali rufaa za wabunge hao kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho wa kuwavua ubunge, haukuwa sahihi.
Chadema imewakilishwa na Wakili Peter Kibatala, John Mallya, Jeremiah Mtobesya na Jonathan Mdeme.Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 13 Juni 2022.
Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA