February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MAHAKAMA YATOA SIKU MOJA WITO WA MBATIA KUPINGA NDUGAI KUJIUZULU KUJIBIWA

James Mbatia-M/kiti NCCR Mageuzi

Na: Anthony Rwekaza

Mahakama Kuu leo Jumatatu Januari 24, 2022 imeahirisha shauri namba 2/2022 lililofunguliwa na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia dhidi ya Job Ndugai na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Katibu wa Bunge.

Ahirisho hilo limekuja kufuatia upande wa wajibu wito kushindwa kuwasilisha majibu yao, huku pia Ndugai ambaye na ni miongoni wanaohusika na wito hakufika Mahakamani wala mwakilishi wake au kutoa taarifa yoyote ya kutofika, kutokana na hali hiyo Mahakama imeulekeza upande wa waleta maombi kumfikishia kwa uhakika taarifa ya wito(summons) ambayo awali wamedai walimfikishia kupitia njia ya barua pepe (Email) baada ya utaratibu wa kutumia ofsi za kibunge kushindikana.

Upande wa wajibu maombi waliiomba Mahakama kuwapatia siku 14 ili kujibu wito, lakini upande wa waleta maombi umepinga hoja hiyo na kuiomba Mahakama kutoa uamuzi wa shauri hilo kabla ya uchaguzi wa Spika unaotarajiwa kufanyika Januari 31, 2022, kufuatia hoja za pande hizo mbili Mahakama imetoa siku moja kwa wajibu wito kuwa tayari wamejibu kufikia Januari 26, 2022 saa 5:00 asubuhi ambapo shauri hilo litasikilizwa tena.

Upande waleta mashtaka unaongozwa na Wakili Boniface Mwabukusi ambapo leo walikuwa jumla ya Mawakili tisa akiwemo Wakili Jeremia Mtobesya huku upande wa waliopokea wito umeongozwa na wakili Mussa Mburu ambapo walikuwa jumla ya mawakili wanne, huku shauri hilo likisikilizwa na majaji watutu

Itakumbukuwa Spika Job Ndugai aliwasilisha barua ya kujiudhulu nafasi ya uspika mnamo Januari 06, 2022 aliandika barua ya kujiudhulu kwenda kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwasilisha nakala yake kwa Katibu wa Bunge.

Mara baada ya kuandika barua hiyo CCM ilitangaza kuridhia kujiudhulu kwa Ndugai na kuamua kuweka wazi mchakato wa awali wa kupata mgombea uspika kwa tiketi ya Chama hicho, ambapo Wanachama 71 walichukua fomu kuwania nafasi hiyo lakini jina la Naibu Spika, Dr. Tulia Ackson lilipitishwa na Chama kuwania nafasi ya hiyo.

Kufuatia michakato hiyo James Mbatia alitinga mahamaka Kuu Dar es salaam Ijumaa Januari 21 kufungua shauri akipinga mchakato uliotumiwa na Ndugai kujiuzulu nafasi aliyokuwanayo akidai umekiuka matakwa ya Katiba inavyomuelekeza kuwa anatakiwa kujiudhulu mbele ya vikao vya Bunge huku pia anapinga mchakato unaoendelea ndani ya vyama wa kupata Spika mpya, ambapo kwa mujibu wa taarifa ya Bunge uchaguzi wa kiti icho unatarajiwa kufanyika Januari 31, 2022.