February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

MAGAZETI MANNE YALIYOFUNGIWA YAFUNGULIWA, WAZIRI NAPE ASEMA NI AGIZO LA RAIS

Na: Anthony Rwekaza

Waziri wa Habari na Mawasiliano ya Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, leo Alhamisi Februari 10,2021 amesema ametoa leseni za kuanza kuchapishwa kwa magazeti ya MwanaHALISI, Tanzania Daima, Mseto na Mawio “Kifungo kimetosha. Kikubwa kazi iendelee,” amesema Nape.

Ameeleza hayo Jijini Dar es Salaam leo katika Kikao na Wahariri wa Vyombo vya Habari na kusema ambapo amesema hatua hiyo imekuja kufuatia kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni kufungua ukurasa mpya, ambapo ameweka wazi magazeti yaliyofunguliwa kuwa ni MwanaHALISI, Mawio, Mseto Tanzania Daima ambayo yote yalifungiwa kwa nyakati tofauti.

“Agizo la Rais ni Sheria,leo nitatoa leseni kwa Mwanahalisi,Mawio,Mseto,Tanzania Daima ambayo yalikuwa yamefungiwa, tuanze kwa kufungua ukurasa mpya Ili tumalize kabisa jambo hili,kifungo kimetosha ” Amesema Waziri wa Habari na Mawasiliano ya Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye

Pia amesema Serikali inalenga kuboresha mahusiano kati yake na wadau wa habari, ambapo amedai Rais Samia Suluhu Hassan ameshaangiz kupitiwa kwa Sheria, Sera, Kanuni na Taratibu zinazosimamia Sekta ya Habari ili kuona namna nzuri ya kuzifanya ziwe rafiki pindi Wanahabari wakiwa Katika utekelezaji wa majukumu

Amesema Serikali itatumia Busara kuhakikisha mambo yanaenda sawa, ambapo amesema kuwa nia ya Serikali ya awamu ya sita ni njema hivyo wanalenga kutengeneza mahusiano na maridhiano mazuri yatakayoongeza mshikamano wa pamoja.

Aidha Waziri Nape Nnauye ameongeza safari ya mabadiliko sio rahisi na inaweza kuchukua muda, amesema licha ya safari hiyo kuchukua muda haimanishi safari safari haitakiwi kuendelea mbele, amedai kuwa wakati mwingine anaweza kwenye safari utokea vikwazo lakini haitakiwi kuacha.

“Najua tulipotoka, wakati mwingine safari ya mabadiliko sio rahisi na inaweza kuchukua muda. Inapochukua muda haimaanishi safari imesimama maana ni rahisi kutuhumiana kutosonga mbele. Wakati mwingine unasafiri unakwenda unakutana na jiwe, ukikutana na jiwe using’ang’anie kulipasua, rudi hatua moja nyuma nenda kushoto au kulia unaenda mbele. Ukirudi hatua moja haimaanishi umeamua kuacha safari, bali unatafuta njia nzuri ya kuendelea na safari” amesema Waziri wa Habari na Mawasiliano ya Teknolojia ya Habari

Vilevile Waziri Nape amesema Serikali kupitia Wizara anayaoingoza wataunda kamati ndogo itakayowajumuhisha Wanahabari ili kushauriana na baada mashauriano hayo kama yatafikia muafaka ya kufanya malekebisho kwenye baadhi ya vifungu katika Sheria ya huduma ya vyombo vya habari (Media Service Act. 2016) watapeleka sheria hiyo Bungeni ili kufanyiwa marekebisho, huku akitaka sheria zilizopo kuzingatiwa wakati wakiendelea na michakato mingine ya marekebisho.

Magazeti hayo yalifungiwa kwa nyakati tofauti kufuatia kudaiwa kuchapisha habari ambazo zilidaiwa ni kinyume na maadili yanayoongoza tasnia ya habari, ikiwemo kuchapisha habari za uongo, uzushi, uchochezi na uzandiki. Lakini baadhi ya wadau wa habari walikuwa na mitazamo mseto juu ya hatua iliyochukuliwa kwa magazeti hayo kufungiwa.

Itakumbukuwa Januari 11, 2017 MCT, LHRC na THRDC zilifungua shauri mbele ya Mahakama ya Afrika Mashariki Shauri Na. 2/2017 wakipinga vipengele mbalimbali vya Sheria ya Huduma ya Habari kuwa vilikuwa vinakiuka mkataba wa Afrika Mashariki na vilikuwa kinyume na misingi ya haki za bainadamu na utawala bora.

Machi 28, 2019 Mahakama ilitoa hukumu na kubatilisha vifungu 7 (3) (a), (b), (c), (f), (g), (h), (i), (j), 19, 20 and 21, 35, 36, 37, 38, 39, 40, 50, 52, 53, 54, 58 na 59 vya sheria hiyo. baada ya uamuzi huo Serikali ilionesha nia ya kukata rufaa mnamo Aprili 11, 2019, lakini nia hiyo ilifutwa na Mahakama hiyo kitengo cha rufaa Juni 9, 2020 baada ya walalamikaji kupeleka maombi.