February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

ACHANGIWA MAMILIONI YA FEDHA BAADA YA KUFUNGWA MIAKA 43 JELA KIMAKOSA.

Kelvin Strickland

Na Leonard Mapuli na Aliya Aziz.

Maelfu ya watu wamemchangia fedha zaidi ya Dola Milioni 1 Mwanaume aliyetumikia kifungo cha miaka  43 jela baada ya kuhukumiwa kimakosa.

Kelvin Strickland (62) mkazi wa eneo la Missouri jijini Cameron nchini Marekani, alihukumiwa miaka 50 gerezani kwa Mauaji .Angali akitumikia hukumu hiyo,Strickland aliendelea kupinga hukumu hiyo na kusema kuwa yeye hakuhusika na mauji hayo yaliyotokea mwaka 1979 jijini Missouri.

Jumanne ya wiki hii,Novemba 23,Jaji kiongozi James Welsh alizifuta hukumu zote za Strickland, na kuamuru aachiliwe huru.

Mara baada ya kuachiwa huru kwa Strickland ,watu waishio jijini Missouri wameanzisha mchango maalumu,uiopewa jina la  “gofundme” kumchangia Strickland ili aweze kumudu maisha yake baada ya kusota jela kwa miaka mingi bila hatia.Hadi sasa jumla ya dola za kimarekani milioni moja zimekusanywa lengo likiwa ni kumpa angalau kiasi cha dola 750 kwa kila mwaka iliosota jela.Kiasi kilichopatikana hadi sasa,ni Zaidi ya malengo ya awali,yaliyolenga kukusanya dola laki 7,500 na hivyo kuvuka malengo kwa ongezeko la dola 2,500..

Kelvin Strickland amesema baada ya kupata habari za mtu aliyeachiliwa huru na kusilikia jina lake kuwa ndilo, alifurahi sana.Kitu cha kwanza alichokifanya  baada tu ya kutoka gerezani, ilikuwa  ni kutembelea kaburi la mama yake aliyefariki angali gerezani

“Baada ya kujua mama yangu amefariki,sikuweza hata kuzuru kaburi lake, iliniuma sana kama ilivyoniuma kuhukumiwa kwa kosa ambalo sikuwa nimefanya”;Amesema Kelvin Strickland kwa majonzi makubwa.

Strickland ,amenukuliwa pia na chombo cha Habari cha CNN cha nchini Marekani akidai kuwahapati hata tone la usungizi,tangu atoke gerezani,kila kitu ni kigeni kwake,hata milio mizuri ya ndege nyakati asubuhi alikuwa ameshaisahau.

Kelvin Strickland  anakuwa mtu wa kwanza aliyesingiziwa kesi na kuhukumiwa kimakosa na kutumikia kifungo cha miaka mingi zaidi jela kuliko mtu yoyote jijini Missouri baada ya kutumikia 93% ya kifungo chake alichohukumiwa akiwa na umri wa miaka 18 tu.