Waziri mmoja nchini Madagascar,Serge Gelle ameogelea kwa saa 12 ili kujiokoa baada ya helikopta aliyoipanda kuanguka baharini wakati wakifanya shughuli ya uokoaji huku Maafisa wengine wawili wa usalama waliokuwa pamoja naye kwenye ndege hiyo nao wamenusurika.
Kwa mujibu wa taarifa zinaeleza kuwa Waziri huyo na maafisa usalama walikuwa wakikagua eneo la Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo mahala ambapo mashua ya abiria ilizama na kusababisha vifo vya watu takribani 39.
Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina ametoa salamu rambirambi kwa waliofariki na kuwapongeza Gelle na maafisa wengine wawili waliowasili kwenye mji ulio kando mwa bahari wa Mahambo baada ya kuogelea kwa saa 12 baada ya ndege kuanguka.
“Ningependa mrushe video hii kwa familia yangu waione, wafanyakazi wenzangu, serikali iione, niko hai na salama,” amesema Gelle.
Mkuu wa polisi, Zafisambatra Ravoavy aliliambia shirika la habari la AFP kuwa Gelle alitumia moja ya viti vya helikopta hiyo kama kifaa cha kuelea.
Habari Zaidi
ETHIOPIA: AJIUNGA CHUO KIKUU AKIWA NA MIAKA 69
MWANDAAJI MISS RWANDA KUFUNGULIWA MASHITAKA YA UHALIFU WA KINGONO
KENYA: ODINGA AMTEUA MARTHA KARUA KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS