February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

M/KITI WA NaCONGO ATEMBELEA THRDC

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NaCONGO),Lilian Badi hii leo ametembelea ofisi za Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania( THRDC) na kufanya mazungumzo na Mratibu wa THRDC,Onesmo Olengurumwa.

Pamoja na mambo mengine wamejadiliana namna ya kuboresha ushirikiano kati ya THRDC na NaCONGO ikiwemo namna wanachama wa Mtandao watakavyoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Asasi zisizo za Kiserikali (AZISE) unaotarajiwa kufanyika juma lijalo jijini Dodoma.

Pichani ni Mratibu THRDC,Onesmo Olengurumwa na Lilian Badi,Mwenyekiti NaCONGO.