February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

LISSU; WANANCHI WA NGORONGORO WANAUMIZWA NA MAAMUZI BILA KUSHIRIKISHWA

Na: Anthony Rwekaza

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu amesema wananchi wa jamii ya Ngorongoro wanaumizwa na maamuzi mbalimbali yanayotolewa kuhusu sakata la Ngorongoro kwa kuwa hawashirikishwi vyema kwenye uamuzi unaotolewa.

Akizungumza na chanzo maalumu cha taarifa, Mwanasiasa huyo amabaye amekuwa akijipambanua kama Mwanaharakati mtetezi wa haki za binadamu, amesema kuwa wananchi wa Ngorongoro wanaumizwa na uamuzi katika sakata linaloendelea, kwa kuwa wamekuwa hawana kauli juu ya maamuzi mbalimbali yanayotolewa.

“Wananchi wa Ngorongoro ambao ndio wanaumizwa na maamuzi katika sakata la Ngorongoro, hawana kauli katika maamuzi yanayotolewa”TunduALissu

Pia Lissu amesema kuwa Shirika la UNESCO limeweka hadharani kuwa haliungi mkono sakata la kutaka kuwaondoa watu jamii ya kimasai wanaoishi Ndani ya hifadhi ya Ngorongoro, ambapo amewataka waliosema kuwa Shirika hilo limeunga mkono wajitokeze hadharani kwa nia ya kuomba radhi.

“Kama Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limesema hadharani haliungi mkono wamasai kuhamishwa, sasa kinachotakiwa twende hatua moja mbele kwa waliosema kuwa UNESCO wameunga mkono hatua hiyo, wajitokeze hadharani na kuomba msamaha” -Tundu Lissu

Aidha Lissu ameeleza kuwa Sera za Serikali ya Kikoloni zilizohusu uhifadhi hususani kwa jamii ya Ngorongoro ulizingatia zaidi utu na huruma ikilinganishwa na sera za Serikali ambazo zimekuwa zikitumika mara baada ya kupata uhuru.

“Ukiangalia sera za serikali ya kikoloni kuhusu uhifadhi ikiwemo watu wanaoishi kwenye hifadhi hususan watu wa Ngorongoro ukilinganisha na sera hizo hizo za serikali baada ya uhuru, utaona kwamba serikali ya kikoloni ilikuwa ina utu na huruma” amesema Malamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu

Itakumbukwa hivi karibuni kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya viongozi wa kimila kutoka kwenye jamii ya kimasai Wilayani Ngorongoro amabao wanaishi katika hifadhi kulalamikia juu ya kutoshirikishwa kwenye baadhi ya vikao muhimu vyenye maudhui ya kujadili sakata la mgogoro huo ambao umekuwa gumzo kwa zaidi ya miezi miwili.

Vilevile wadau amabao ni Watetezi wa Haki za Binadamu ikiwemo Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini Tanzania, (THRDC), kituo cha Sheria na Haki za Binadamu,( LHRC) pamoja na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali yamekuwa yakishauri Serikali kutatua sakata hilo kwa mfumo shirikishi wa kimaamuzi ikiwemo kuwapana nafasi wananchi kutoa maoni yao.

Hata hivyo Serikali kupitia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt. Damas Ndumbalo wamekuwa wakieleza kuwa wanashirikiana vyema na jamii hiyo ikiwa ni pamoja na kufanya vikao na wananchi pamoja na viongozi wa kimila wa jamii ya kimasai kutoka Ngorongoro, lakini licha ya maelezo yao bado kumekuwepo na malalamiko juu ya jamii hiyo kutoshirikishwa ipasavyo.

Kwa umuhimu ikumbukwe kumekuwepo na madai kuwa Serikali inataka kuwaondoa wananchi wa Ngorongoro, kuwaamisha maeneo mengine ikiwemo Handeni ambapo inadaiwa tayari zinajenga nyumba kwa ajili ya kaya mbalimbali kuamia huko ikiwa Serikali imedai kuwa zoezi la watu kuama sio la lazima isipokuwa wanaama kwa hiari, imekuwa ikielezwa na viongozi wa Serikali pamoja na baadhi wadau kuwa watu na idadi ya mifugo kwenye hifadhi hiyo imeongezeka hali ambayo wanadai inaweka lehani hifadhi hiyo.

Lakini hoja hizo zimekuwa zikipingwa vikali na baadhi ya wadau kuwa hazijabeba utafiti wa kitaalamu na isipokuwa ni hoja zenye propaganda hasi nyuma ya pazia ambazo haitaki kuwekwa wazi. Ambapo wadau hao wanadai kuwa kitendo cha kuwaondoa wanachi hao kwa nguvu ya aina yoyote au kwa kutumia hoja zinazotolewa ikiwemo kuwa wanishi maisha magumu ni jambo ambalo linakiuka sheria na misingi muhimu ya haki za binadamu.