February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

LISSU AWEKA WAZI MAAMUZI MATATU MAZITO YA KAMATI KUU YA CHADEMA

Na Antony Benedicto

Kufatia Jeshi la Polisi kuwashikiria baadhi viongozi na wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe, kiliitishwa kikao cha dharula cha Kamati kuu kujadili jambo hilo.

Kikao hicho kilichofanyika jana alihamsi Julai 22, kimeibuka na maazimio matatu ambayo wamepanga kuyatekeleza hayo yamebainishwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu.

” Kamati kuu ya kwenye kikao cha dharula imeazimia kuchukua hatua zifuatazo, kwanza imeunda kamati itakayoendesha kampeini ya kimataifa Duniani kote, kuileza Dunia kuiambia huyo tumdhaniaye ni tofauti na Rais Magufuli anaweza akawa zaidi ya Rais Magufuli” amesema Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu

Makamu Mwenyekiti huyo aliogeza kuwa watazunguka kwenye mabunge ya Mataifa ya nje na kukutana na wafanyabiashara kuwaeleza mazingira ya biashara ya Tanzania sasa, huku yeye akisema atakuwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo , pia ameeleza azimio la pili.

“Itaundwa Kamati ya ndani ya Nchi ambayo itakuwa kwa ajili kuratibu shughuli zote za kutafuta Katiba mpya kwa Nchi yetu, kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wale wote ambao wameonewa kwa sheria za kikandamizaji na kwa kesi za kubumba wanapata msaada, kampeini ya Katiba mpya itaedelea, kongamano la Katiba Mwanza litafanyika liko pale pale, tutapanga tutarudi Mwanza kwenda kufanya kongamano kama inavyoruhusiwa na sheria za Tanzania” amesema Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu

Tutafanya mikutano na makongamano ya aina hiyo Nchi nzima, kumkamata Mwenyekiti na kumfungulia makosa ya Jinai ya Ugaidi hayatatuzuia sisi wala kutukatisha tamaa ya kuendeleza madai yetu halali ya kuipatia Nchi yetu Katiba mpya” amesema Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu

Aidha Makamu Mwenyekiti huyo ambaye anaishi nje ya Nchi kwa kile anachodai kuwa ni kwa sababu za usalama wake ameshiriki kikao hicho kwa njia ya mtandao (video conference), amebainisha azimio la tatu lililoazimiwa na Kamati Kuu kuwa lazima jitihada walilizo zianzisha ziendelee.

” Kamati Kuu imeazimia kwamba hizi jitihada za ndani na nje lazima ziendelee na mapambano ya kudai Katiba mpya lazima yaendelee” amesema Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu

Kamati Kuu hiyo imetoa maadhimio hayo zikiwa tayari zimepita siku mbili tokea baadhi ya viongozi na wanachama wa CHADEMA waliposhikiriwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza usiku wa manane kuamkia jumatano Julia 21,2020, huku Mwenyekiti wa chama hicho akasafirishwa mpaka Dar es Salaamu kabla kuibuka sintofahamu kuhusu wapi halipo lakini Jeshi la Polisi lilitoa taarifa ya kushikiriwa kwake.