February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

LHRC YALAANI VIKALI JARIBIO LA KUTAKA KUMKATA MKONO MWENYE UALBINO

Na: Anthony Rwekaza

Kufuatia taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari mbalimbali ya kushambuliwa kwa mtu mmoja, ayetambulika kwa jina la Mohamed Rajabu ambaye ni alibino Mkazi wa Kata Mabibo Jijini Dar es Salaam , Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC) kimetoa tamko ya kulaani tukio hilo, huku kikiwataka Serikali kupitia Jeshi la Polisi kuwakamata watumiwa na kufanya upelelezi wa tukio hilo kabla ya hatua nyingine za kisheria.

Akizungumza na vyombo vya habari leo April 26, 2022 Mkurugezi Mtendaji LHRC, Anna Henga amesema kuwa baada ya kusambaa kwa taarifa hiyo hususani kwenye mitandao ya kijamimii LHRC walichukua hatua ya kufanya tafiti ili kubaini ukweli juu ya taarifa hiyo, amedai kuwa baada ya kufanyika kwa utafiti huo walibaini kuwa taarifa hiyo ni yakweli licha ya bado kutodhibitishwa na Jeshi la Polisi.

” Baada ya taarifa hizi kusambaa katika mitandao ya kijamimii Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilichukua hatua ya kufanya utafiti ili kubaini ukweli juu ya taarifa hii ya kusikitisha, ambapo kwa mujibu wa utafiti wa LHRC tumebaini kuwa taarifa hizi ni za kweli licha ya kutodhibitishwa na Jeshi la Polisi mpaka sasa” amesema Mkurugezi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga

Amesema kuwa kwa mujibu wa mashuhuda my akiwemo wanafamilia ni kuwa watuhumiwa hao walijaribu kutaka kumkata mikono yake kitendo ambacho kitendo ambacho hakikufanikiwa Kwa asilimia mia moja, lakini amedai kuwa walifanikiwa kumjeruhi kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Pia Mkurugezi Mtendaji huyo amesema kuwa kwa kipindi cha takribani miaka mitano kuanzia mwaka 2015 mpaka mwaka 2020 hakukuwa na ripoti yoyote ya mauaji dhidhi ya watu wenye ualbino. Amedai kuwa hali hiyo ilichangiwa na juhudi za vyombo mbalimbali vinavyosimamia masuala ya haki, ikiwemo Jeshi la Polisi, Asasi za Kiraia, Tume ya Haki za Binadamu na Mahakama kuwachukulia hatua kali za kisheria.

“Kwa kipindi cha takribani miaka mitano, kuanzia mwaka 2015, mpaka 2020 hakukuwa na ripoti yoyote ya mauaji dhidhi ya watu wenye ualbino. Hii ni baada ya Juhudi za Jeshi la Polisi Tanzania, Mahakama, Asasi za Kiraia na Tume ya Haki za Binadamu Nchini kufanya juhudi kubwa katika kukemea, kuwakamata wahusika na kuwapa adhabu kali kwa mujibu wa sheria.”amesema Mkurugezi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga

Aidha katika tamko hilo wametoa wito wao kwa mamlaka mbalimbali kuchukua hatua za haraka ili kukomesha matukio hayo, ambapo wamelitaka Jeshi la Polisi na Serikali kuhakikisha watuhumiwa waliohusika na tukio hilo wanakamatwa na kuchuliwa hatua.

” Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi na Serikali kuhakikisha kuwa watuhumiwa wa kesi hii wanakamatwa, upelelezi unafanyika kwa wakati na kufikishwa mahakamani na kupatiwa adhabu kali ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.”amesema Mkurugezi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga

Vilevile wametoa wito wao kwa mamlaka kupanua upelelezi wa kesi za matukio ya aina hiyo kwa watu wenye ualbino ili kuwakamata wahamasishaji wa soko haramu la viungo vya watu wenye ualbino ambao ametaja kuwa ni baadhi ya waganga wa kyenyeji na wanaoamini imani za kishirikina ili kuchukuliwa hatua kali.

Hata hivyo pia wametoa wito kwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Asasi za Kiraia, kurudisha upya juhudi za pamoja na mikakati na ya kukemea vitendo vya ukatili kwa watu wenye ualbino, ambapo amedai kuwa kurudi upya kwa matukio hayo mfululizo kunaashiria kurudi hali nyuma kabla ya mwaka 2015.

Lakini katika juhudi za kukomesha matukio mbalimbali kwa watu wenye ualbino wameitaka jamii kwa ujumla kuwa mstari wa mbele katika kukemea matukio hayo, huku wakiwataka wananchi kuheshimu Haki za watu wenye ualbino na kutambua kuwa kufanya ukatili dhidhi yao ikiwemo kukata viungo vyao ni kosa la kwa mujibu wa sheria ya ya kanuni ya adhabu sura ya 16, kifungu cha 225.

Katika kueleza mfululizo wa matukio hayo katika tamko hilo Mkurugezi Mtendaji LHRC amesema kuwa May 2021 Mkoani Tabora kulitokea tukio la mauaji ya kikatili kwa mtoto mwenye ualbino, ambaye inadaiwa mwili wake ulitolewa baadhi ya viungo vyake ikiwemo mikono, pia wamesema kuwa November 2021 kulitokea tukio lingine Mkoani Tanga Wilayani Lushoto likihusisisha imani za kishirikina, ambapo wamedai kuwa mwili wa marehemu ambaye alikuwa albino ulifukuliwa na baadhi ya viungo kuchukuliwa.

Itakumbukwa awali kabla ya mwaka 2015 yalikuwa yakiripotiwa mara kwa mara matukio ya mbalimbali ya ukatili dhidhi ya watu wenye ualbino, hata hivyo Serikali pamoja na wadau wa Haki za Binadamu walijitokeza adharani na kukemea vikali matendo hayo ambayo uhusishwa na imani za kishirikina.