February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

LHRC WALAANI TUKIO LA MAUAJI LINALODAIWA KUTENDWA NA POLISI, WASHAURI MAMBO MATATU

Na: Anthony Rwekaza

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Nchini (LHRC) kimelaani tukio linalodaiwa kufanywa na askari Jeshi la Polisi lilopelekea kifo chaJuma Ramadhani (35) kilichotokea Machi 14, 2022 na kusababisha kujeruhiwa kwa watu Omary Amdani (35) na Bwana Nasibu Moshi (35), katika uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma, kwa kupigwa risasi wakati Jeshi la Polisi likijaribu kidhibiti vurugu zilizohusisha mashabiki wa timu ya Mwandiga FC dhidi ya Kipampa FC.

Katika tamko lao lililotolewa leo Machi 16, 2022 wamesema kuwa licha ya Jeshi la Polisi kuwa na mamlaka kisheria kutuliza ghasia, lakini wamedai kuwa Jeshi hilo bado linabaki na wajibu wa kuzingatia na kuheshimu misingi, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali ya utendaji kazi wa Jeshi hilo ikiwemo Mkataba wa umoja wa Mataifa wa ‘Matumizi ya Nguvu na Silaha wa Mwaka 1990 pamoja na ‘ Mwongozo wa Utendaji Kazi wa Jeshi la Polisi (PGO) Marejeo ya Mwaka 2021.

Pia katika tamko hilo wamesema kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na mikatamba mbalimbali ya kimataifa na kikanda ambayo Tanzania imeridhia vimeeleza kuwa haki ya kuishi ni haki ya msingi hisiyopaswa kuingiliwa na chombo chochote cha dola.

“kwa mujibu wa Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na mikatamba mbalimbali ya kimataifa na kikanda ambayo Tanzania imeridhia inaweka bayana kuwa haki ya kuishi ni haki ya msingi hisiyopaswa kuingiliwa na chombo chochote cha dola.” Taarifa hiyo imeeleza

Aidha kituo kituo hicho ambacho ujihusisha na majukumu ya mbalimbali ya utetezi wa haki za binadamu, kimesikitishwa na muendelezo ya matukio mbalimbali yanayoendelea kutokea na kulihusisha Jeshi la Polisi, ambapo tamko ilo linadai kua tukio hilo limetokea siku chache mara baada ya Katibu wa itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kutoa malalamiko juu ya mwenendo wa Jeshi la Polisi Polisi kupitia vyombo vya habari, ambapo alishauri kuundwa kwa Tume maalumu ya kuchunguza mwenendo wa Jeshi hilo.

Lakini pia tamko ilo limeeleza kuwa tukio hilo limetokea ikiwa ni siku chache mara ikiwa imepokelewa ripoti ya Kamati iliyokuwa inachunguza mauaji ya mfanyabiashara aliyedaiwa kuawa na askari Polisi Wilayani Kilindi Mkoani Mtwara mnamo Februari 26, 2022.

Katika tamko hilo LHRC wametoa wito kwa Serikali, ambapo wametaka hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi ya maafisa wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Hata hivyo wameshauri kuundwa kwa Tume huru ya kuchunguza kifo cha mtu huyo, huku pia wakishauri kuundwa kwa chombo maalumu kwa ajili ya kuchunguza malalamiko dhidi ya Jeshi la Polisi Nchini.

Itakumbukwa tamko hilo limekuja siku moja baada Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma, kupitia Kamanda wa Jeshi la Polisi Kigoma, Jwmes Manyama, kuthibitisha taarifa hiyo kuwa askari namba F. 5123 D/ACPL Subira, alifyatua risasi zilizopelekea kusababisha kifo cha raia Juma Radhani, na majeruhi wawili, amabapo alidai kuwa askari huyo alikuwa akijitetea kutoka katika mashambulizi ya mashabiki waliokuwa wanamshambulia kwa mawe katika Uwanja wa Lake Tanganyika, mkoani humo.

Kamanda Manyama amesema, Subira alifyatua risasi hizo akijihami kunyang’anywa silaha na mashabiki hao waliokuwa wanamahambulia akiwa chini. Ambapo ilikuwa mechi ya fainali ya kombe la Dk. Livingstone, kati ya Mwandiga FC na Kipamba FC