February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

KUTOONGEZEWA MUDA MKANDARASI WA BWAWA LA UMEME

Na Neima Kisanga

Shirika la umeme Tanzania (Tanesco), alitamuongezea muda Mkandarasi wa Kampuni ya Arab Contractor pamoja na Kampuni ya Elsewedy Electric kutoka Misri wanaojenga bwawa la kufua umeme wa megawati 2,115 wa Julius Nyerere pamoja na kuomba kuongezewa muda
Alisema hayo Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo , Dk Titto Mwinuka akiwa pamoja na timu ya Mkurugenzi na Makamishna wa wizara ya fedha wakiwa wametembelea mradi huo uliopo katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji Wilayani Rufiji Mkoani Pwani

Dk Mwinuka alilazimika kuongea hayo baada ya kuulizwa swali na Makamishna wa Wizara ya fedha

Tumekuwa tukitoa ushirikiano wa Hali ya juu na Mkandarasi wa mradi huu na tunatarajia kuona ujenzi wote unakamilika kwa muda mwafaka na hatutokubali kuongeza muda mwingine, nukuu ya Dk Mwinuka.