February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

KUTOKA KUWA KIONGOZI WA MIGOMO YA WANAFUNZI HADI KUWA RAIS WA CHILE.

Gabriel Boric-Rais Mteule wa Chile.

Mgombea urais kupitia Chama cha Mrengo wa Kushoto nchini Chile,Gabriel Boric,ameshinda kiti cha urais,katika duru ya pili ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumapili Disemba 19.Boric,ameshinda kwa 55.87% mbele ya mpinzani wake mkuu Jose Antonio Kast wa Chama cha Republican,aliyepata 44.13%.

Boric (35)anakuwa rais wa kwanza kijana,tangu nchi hiyo iingie kwenye mfumo wa kufanya Chaguzi za Kidemokrasia,mwaka 1990.

“Kuanzia leo,ndiye rais wetu mteule,anastahili heshima na apewe ushirikiano”,ameandika Kast katika ukurasa wake wa Twetter,mara baada ya Idara ya huduma za Chaguzi nchini Chile,kutangaza matokeo usiku wa kuamkia leo,Disemba 20.

Jose Antonio Kast-Mgombea aliyeshindwa Urais Chile

Kwa mujibu wa katiba ya nchi ya Chile,Rais Mteule ataapishwa April 11 mwaka 2022 kuchukua nafasi ya Rais wa sasa, Sebastián Piñera,aliyehudumu mihula miwili tofauti ya urais,yaani Rais wa 33 Chile (2010-14)na Rais wa 35 (tangu 2018) hadi sasa.