March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

KITUKO:MWANAMKE AFUNGA NDOA NA “ROHO MTAKATIFU”

Bibi Elizabeth akiwa na mume wa zamani baada ya kufunga ndoa na Roho Mtakatifu.

Katika hali isiyo ya kawaida,mwanamke Elizabeth Nalem mwenye umri wa miaka 41 na mama wa Watoto si amemkataa mumewe Joshua Nalem kwa madai kuwa sasa anaolewa na “Roho Mtakatifu,limeripoti jarida la the Nation,la nchini Kenya.

Elizabeth,mkazi wa Makutano katika Kaunti ya Pokot  Kaskazini nchini Kenya ambae pia ni mtumishi wa umma amemshangaza mumewe napamoja na wakazi karibu wote wa eneo hilo baada ya kuanda sherehe katika hoteli ya Chelang’a mjini Makutano kusherekea harusi yake aliyofunga pingu za Maisha mpya na Roho Mtakatifu.

Katika tukio hilo la aina yake,Elizabeth alisindikizwa na wafanyakazi wenzake Pamoja na wafanyabiashara waliomshangilia alipokula kiapo cha kuoana na Roho Mtakatifu ambae hakuwepo eneo la kiapo.

Ndoa hiyo imefungishwa na Mchungaji Albert Rumaita wa kanisha Anglican anayehudumu eneo la Makutano.Mbele ya mume wake wa zamani ambae alikuwa amepigwa butwaa pamoja na watu wengine,Elizabeth alisema “Nipo Tayari” kuolewa na Roho Mtakatifu.

“Nimeitumikia dunia muda wote wa Maisha yangu,lakini sasa Roho Mtakatifu kaniomba nimtumikie Mungu,na amenileta kwa Mchungaji Rumaita ambae ndiye kaninunulia hata hii shera na kunigharamia kila kitu hapa”,amesema Elizabeth wakati wa sherehe yake.

Mume wa zamani wa Elizabeth aliyeishi nae miaka 20 na kuzaa watoto sita ameonesha mshangao mkubwa.

“Nilimtolea mahari ya ng’ombe 22 na mbuzi 15 lakini sasa eti ameolewa na roho Mtakatifu?siamini”,amesema Joshua Nalem,aliyekuwa mume wake.

Kwa mujibu wa imani ya Kikristo,Roho Mtakati ni nafsi ya tatu na sehemu ya utatu mtakatifu, unaoundwa na Mungu baba,Mungu Mwana na Roho mtakatifi (Trinity) na wote hawa hawaonekani kwa macho bali imani, lakini mama huyu amedai kufunga ndoa na Roho Mtakatifu.

Katika ndoa hiyo iliyofungwa Jumanne Mei 25,mfungishaji wa ndoa Mchungaji Rumaita alisema amechukua uamuzi huo kwa kile alichokiita huenda ni mwisho wa dunia na kwamba ameamua kumfanya Elizabeth kutimiza ndoto yake ya kuolewa na Roho Mtakatifu.