February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

KINY’ANGANYIRO WAJUMBE NACONGO WILAYA ZA UBUNGO,KINONDONI CHAMALIZIKA

Wajumbe wapya NaCongo (W) ya Ubungo wakiwa pamoja na viongozi

Na Leonard Mapuli/Hilda Ngatunga

Baraza la Taifa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NACONGO) linafanya uchaguzi kupata wajumbe kutoka ngazi ya wilaya watakaowakilisha katika uchaguzi ngazi ya mkoa hadi taifa.Zoezi hilo linafanyika kote nchini  leo June 26.

Watetezi Tv imefanikiwa kushuhudia zoezi hilo katika Manispaa za Ubungo, na Kinondoni  katika uliotawaliwa na utulivu  pamoja na uwazi mkubwa huku wagombea sita wakiwa wamechukua fomu kuwania nafasi 3 za uwakilishi.

Awali msimamizi wa uchaguzi huo  Bi.Juliana Renatus Kibonde ambae pia ni Msajili Msaidizi wa Asasi katika Manispaa ya Ubungo amesema mgombea mmoja (Edina Shaban Mwalukisa) alienguliwa katika kinyang’anyiro hicho baada ya kukosa vigezo vilivyoweka  na baraza hilo,hivyo kufanya idadi ya wagombea kuwa watano.

Baada ya zoezi la upigaji kura kumalizika na baadae kura kuhesabiwa,msimamizi wa uchaguzi huo alitangaza matokea ambapo mgombea wa kwanza Kelvin Deo Roy alipata kura 1,Charles Philbert Kagugisha kura 1,Chamalo Dente Tanda kura 2,Joseph Yohana Kilomile kura 2,na Lilian Mbaga Liundi kupata kura 4.

Kwa matokeo hayo,msimamizi wa uchaguzi huo amewangaza Lilina Mbaga Liundi, Joseph Yohana Kilomile na Chamalo Dente Tanda kuwa wajumbe wa NACONGO kutoka Manispaa ya Ubungo wataokwenda kuwakilisha katika uchaguzi ngazi ya Mkoa.

Tayari wajumbe hao wamekula kiapo mbele ya msimamizi na wadau wengine walioshiriki uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Tunu Social Hall uliopo Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam.

Mmoja ya wagombea waliojitosa Kinondoni,Perpetua Senkoro akifuatilia zoezi lilivyoendeshwa.

Katika hatua nyingine pi Watetezi media imeshuhudia uchaguzi wa wajumbe wa baraza hilo katka wilaya ya Kinondoni ambapo wagombe tisa wamejitosa kuwania  nafasi  za ujumbe ambapo baada zoezi la kupiga kura na kuhesababu kukamilika,Lulu Ngw’anakilala (kura 12),Marcela Francis Lungu (kura 10),na Henga aliyepata( kura 10) walitangazwa washindi katika uchaguzi  huo.