February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

“KINONDONI KINARA WA UHALIFU”-IGP SIRRO.

IGP Simon Sirro akizungumzia kuhusu uhalifu kushamiri Kinondoni leo Mei 26.

Mwandishi wetu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, ameutaja mkoa wa Kipolisi wa  kinondoni kama kinara wa uhalifu nchini ambapo matukio ya uporaji, uvunjaji wa kutumia nguvu na uporaji kwa kutumia pikipiki yakiwa yameongezeka huku uhalifu mwingine mkubwa wa kutumia silaha za moto ukiwa umeshuka.

IGP Sirro amesema hayo jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na Wenyekiti wa Serikali za Mitaa, watendaji Kata, pamoja na watendaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi ambapo amewataka watendaji wote kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha usalama unaendelea kuimarishwa.

Aidha, IGP Sirro ametoa muda wa wiki moja kuhakikisha wanakomesha vya kihalifu kwa kushirikiana na watendaji wengine huku akitoa wito kwa mgambo kuacha kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa.

“Tutaendelea kutekeleza wajibu wetu kwa kuzingatia uzalendo, taratibu na kanuni na kuhakikisha maeneo yatu na wananchi tunaowahudumia yanakuwa salama”,amejibu Mohamed Mawal, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tegeta huku Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mlalakuwa Suleiman Masare, akiahidi kutoa pikipiki mpya kwa Kituo cha Polisi Chuo Kikuu itakayosaidia kurahisisha utoaji wa huduma za kipolisi kwa wananchi.

Kabla ya kukutana na watendaji wa serikali za mitaa na watendaji wa kata na watendaji wa vikundi vya ulinzi shirikishi pia IGP Sirro, alifanya kikao kazi na maofisa na askari wa Jeshi hilo ambapo aliwataka kuendelea kutimiza wajibu wao na kuwachukulia hatua kali wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu.