February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

KINACHODHANIWA BOMU CHAUA WATOTO WAWILI KAGERA

Revocatus Malimi-RPC Kagera.

Watoto wawili Daniel Joseph (14) na Charles Njola (16)  wakazi wa kijiji cha Mugera kata ya Nyantakara wilayani Biharamulo mkoani Kagera.
wamethibitishwa kupoteza maisha baada ya kulipukiwa na kitu kinachodaiwa kuwa bomu.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi, amesema kuwa tukio hilo lilitokea Mei 27 mwaka huu kati ya saa 12 na saa 1:00 jioni, wakati watoto hao wakirejea nyumbani kutoka malishoni walikokwenda kuchunga ng’ombe.

Amesema kuwa watoto hao waliokota chuma  ambacho kinadhaniwa kuwa ni bomu na bila kujua walianza kukichezea kabla hakijalipuka.

Kutazama video ya tukio hili bofya link hii:https://youtu.be/1skBMNgQ5_M