December 4, 2022

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

KIM MAJI YA SHINGO,NCHI YAKE YAKABILIWA NA NJAA.

Kikao

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ameonesha wasiwasi wa nchi yake kukabiliwa na janga la njaa muda wowote kufuatilia mabadiliko makubwa ya tabianchi,athari za janga la corona,Pamoja na kusitishwa kwa biashara baina yake na China.

Katika Kikao na Chama cha Wafanyakazi cha Korea,Kim amesema hali ya upatikanaji wa chakula nchini humo ni tete.

“Hali ya chakula kwa watu ni mbaya,sekta ya kilimo imeshindwa kubuni mbinu za uzalishaji unaoendana na hali ya hewa baada kimbunga cha Typhoon kutuathiri kwa kiasia kikubwa mwaka jana”,amesema Kim alipozungumza na kamati kuu ya chama cha wafanyakazi iliyokutana kujadili  namna ya kuinua  sekta ya kilimo na uzalishaji.

Janga la Corona ni moja kati ya sababu za uhaba wa chakula nchini Korea Kaskazini baada ya mpaka wa nchi hiyo na China kufungwa ili kuzuia maambukizi mapya ya virusi hivyo baada ya nchi hiyo kushindwa kutoa takwimu za ugonjwa huo.China imekuwa mbia mkubwa  wa biashara na Korea  Kaskazini kwa muda mrefu.

Imearifiwa kuwa Kim amewambia wanachama wa chama chake kuwa masharti ya kutotoka huenda akayaongezea kipindi kirefu Zaidi kwa sababu ya mwenendo wa janga hilo unavyoendelea.

Kim kwa nyakati tofauti amekuwa akinukuliwa akidai kuwa nchi ya Korea Kaskazini haijawahi kukumbwa na janga la Covid-19,kauli ambayo imekuwa ikipingwa vikali na wataalamu wa masuala ya afya.

Ikumbukwe Korea Kaskazini ina miundombinu mibovu ya huduma za afya na uhaba mkubwa wa dawa za binadamu ambapo wachambuzi wanadai taifa hilo haliwezi kuwa salama kwa namna yoyote.

Wakati wa gwaride kubwa  lililofanyika mwaka jana katika mji wa Pyongyang,Kim aliomba radhi kwa wananchi wake kwa kutokuwajibika kikamilifu katika baadhi ya changamoto zinazolikabili taifa hilo ikiwemo janga la Corona.

Licha ya vikwazo mbalimbali vya uchumi ilivyonavyo Korea,uchumi wa viwanda umekua kwa 25% kutoka waka jana,hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na KCNA.

Kwa mara ya mwisho,Korea Kaskazini iliwahi kukumbwa na baa baya la njaa mwaka 1990 ambapo maelfu ya raia wa nchi hiyo.