February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

“KIKWETE YUKO SALAMA”-RIDHIWANI KIKWETE

Tweet ya Ridhiwani Kikwete-Mei 27

Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete amekanusha taarifa za “Sintofahamu” zilizosambaa kupitia mitandao ya kijamii zikimhusishia baba yake mzazi na rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete.

Ridhiwani amesema afya ya rais mstaafu haina dosari yoyote na kwamba yupo salama na anaendelea na shughuli zake za Kila siku.

Kauli ya Ridhiwani imetokana na  yeye mwenyewe binafsi kupokea simu na jumbe mbali mbali kumuuliza kuhusu uhai na usalama wa baba yake kufuatia taarifa za uzushi zilizochapishwa mitandaoni na kuzua taharuki

“Yupo salama wa Afya Nyingi sana. Hana tatizo lolote kiafya na anaendelea na majukumu yake. Taarifa za aina yeyote ni za Kipuuzi na za kupuuzwa”,inasomeka sehemu ya  taarifa ya Ridhiwani aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa twitter.