March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

KIKOSI KAZI KITASAIDIA KULETA MARIDHIANO – JK

Na Mwandishi Wetu

RAIS Mstaafu wa Tanzania, Daktari Jakaya Kikwete, imeupongeza uamuzi wa Rais Samia wa kuunda kikosi kazi Cha kufanyia kazi mapendekezo ya uimarishaji demokrasia ya vyama vingi, akisema utapunguza joto ndani ya nchi na kuleta maridhiano.

Dk. Kikwete ametoa kauli hiyo Leo Ijumaa, muda mfupi baada ya kuwasilisha mapendekezo hayo kwenye kikosi kazi hicho kinachoongozwa na Mwenyekiti wake, Profesa Rwekaza Mukandala.

“Nampongeza Rais Kwa kuunda kikosi kazi ni uamuzi wa busara utasaidia kupunguza joto ndani ya nchi, itasaidia kuleta maridhiano na mwenendo mzuri wa kuendesha siasa nchini,” amesema Dk. Kikwete.

Kwa upande wake, Prof. Mukandala, amesema wako katika hatua za mwisho za ukusanyaji maoni na mapendekezo hayo, Kisha wataandaa ripoti Kwa ajili ya kuiwasilisha kwa Rais Samia.

” Tumeendelea kukusanya maoni kwa wadau mbalimbali Leo tulikuwa na Rais wa Awamu ya Nne, ametoa ufafanuzi na maarifa yake kutokana na uzoefu wake. Sasa hivi hatua tuliyofikia tunachakata yote ambayo tumekusanya, kitafakari na kitayarisha rasimu au ripoti ambayo tutawasilisha Kwa Rais muda ukifika,” amesema Prof. Mukandala.