Watu watatu akiwemo aliyekuwa dereva wa kampuni ya kichina iliyokuwa ikijenga barabara ya Kasulu Kidahwe wamehukumiwa addhabu ya kunyongwa hadi kufa na mahakama kuu kanda ya Kigoma .
Kesi hiyo ya mauaji namba 36 ya mwaka 2020 kosa lililotendeka tarehe 02/10/2016 katika eneo la Kwaga Kasulu mkoani Kigoma likiwajumuisha watu watatu wajulikao kwa majina ya Nuru Venevas,Seth Simon na Ezekiel Kalobezi kinyume na kifungu cha 196 na 197 cha sharia ya kanuni ya adhabu sura ya 16 marejeo ya mwaka 2019.
Akisoma maelezo ya kesi hiyo kabla ya kutoa hukumu jaji wa mahakama kuu kanda ya Kigoma Jaji Athuman Matuma amesema upande wa jamuhuri ukiongozwa na wakili Robert Magige ulikuwa na mashahiiidi 8 na vielelezo huku upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Aliki Saiki.
Nikwamba siku ya kutekeleza mauaji hao washtakiwa wote watatu walihusika kupanga njama ya kushirikiana kuiba kifaa cha exavetor kilichotajwa kwa jina la control box katika mtambo wa gari lililokuwa likiendeshwa na mmoja wa mshtakiwa na katika harakati za kuiba walinzi wengine ambao nao walitajwa kuujua mpango huo walikimbia na kubakia mlinzi aitwaye Richard Chija akipambana nao.
Anasema baada ya mapambano hayo mlinzi huyo alipata majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake na kupoteza maisha baada ya damu nyingi kuvuja kwa mujibu wa daktari aliyefanyia uchunguzi mwili huo ambaye alikuwa moja ya shahidi upande wa jamuhuri.
Akielezea ushiriki wao katika mauaji hayo Jaji Matuma licha ya kwamba kielelezo kilikamatwa kwa mshtakiwa namba mbili Seth Simon lakini uliwezeshwa na maelezo yaliyoendana baina ya washtakiwa watili ambao mmjoja alimtaja jina na kusema kifaa hicho anacho na mwingine kuelekeza sehemu alipo ambapo baada ya kufuata taratibu za upekuzi alikutwa nacho kikiwa chumbani kwa kaka yake mkoani Geita alikokuwa ameenda .
Maelezo waliyotoa polisi washtakiwa na kuwezesha kupatikana kwa kifaa hicho ambacho kilitambuliwa kwa namba na kuwaka kiliporudishwa kwenye mtambo huo washtakiwa waliyakataa mahakamani kwa kueleza waliyaandika kwa kulazimishwa na kupigwa na jeshi la polisi jambo ambalo jaji Matuma aliliona halina mashiko kutokana na kubeba ukweli wenye hatia ambao unaukweli unaoendana .
Hivyo jaji Matuma akasema mahakama hiyo imejiridhisha kuwa washtakiwa wote wanahatia na kila mmoja amehukumiwa kunyongwa hadi kufa.
Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA