February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

KIGOGO BUNGE LA MAREKANI, ATOA TAMKO ZITO KUSHIKILIWA MBOWE NA WENZAKE 11

Na Antony Benedicto

Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje(Afrika) kwenye Bunge la Wawakilishi la Marekani, Kareen Bass ameguswa na kukamatwa kwa viongozi wa kisiasa Tanzania, Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe na wengine 11.

Kareen amesema mamlaka za Tanzania zinatakiwa kuacha kukandamiza vyama vya upinzani na viongozi wake.

Jeshi la Polisi kupitia msemaji wao, wamekili kumshikilia Mwenyekiti wa (CHADEMA), Freeman Mbowe Kanda maalumu ya Dar es Salaam akituhumiwa kwa makosa ya Ugaidi ikiwepo kuhusika kula njama za mauaji ya viongozi sita wa Serikali, pia watuhumiwa wengine 11 wa makosa tofauti wameshikiriwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza.