February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

KESI YA UCHAGUZI NGORONGORO YATOLEWA HUKUMU

Hukumu ya kesi ya uchaguzi namba 42 ya mwaka 2020, imetolewa na mahakama ya Wilaya ya Ngorongoro na kuwakuta watuhumiwa wawili (Paulo Olru na Gabriel Leyami) na kesi ya kujibu huku watuhumiwa wengine watatu (Meshuku Lestik, Tubulu Masiyaya na Daniel Orkery) wakiachiwa huru.

Akizungumza na Watetezi TV Wakili wa Watuhumiwa hao Onesmo Olengurumwa ameeleza kuwa Watuhumiwa hao walishitakiwa kwa kosa la kufanya vurugu, pamoja na kuwashambulia kwa fimbo na mawe na kuwasababishia maumivu makali Anna Cosmas na Lemboya Olesingolio kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.

Kutokana na watuhumiwa kukutwa na majeraha ya risasi, Hukumu imewataka watuhumiwa hao kulipa faini ya shilingi laki 1 (100,000/=) kwa kosa la kufanya vurugu, au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja, na kosa la pili ya Kufanya vurugu na kupasua masanduku ya Kura wametakiwa kulipa faini ya shilingi laki 2 (200,000/=) kila mmoja, Washitakiwa wote wamefanikiwa kulipa faini na kuachiliwa huru.
Wakili Onesmo Oengurumwa ameeleza kuwa mara tu baada ya kutoka kwa nakala ya hukumu kutakuwepo na mchakato wa kuangalia iwapo watakata rufaa “Tunasuburi nakala ya hukumu tuone uwezekano wa kukatia rufaa za hao wawili” Wakili Onesmo Olengurumwa