March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

KESI YA MBOWE:SHAHIDI WA TATU (JAMHURI) AANZA KUTOA USHAHIDI.

Mbowe na wenzake wakifikishwa Mahakamani.(Picha:Maktaba)

Na Leonard Mapuli.

Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi,leo Oktoba 29,imeendelea kusikiliza kesi namba 16/2021,dhidi ya Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Shahidi wa tatu upande wa Jamhuri, Koplo Hafidh Abdallah Mohamed kutoka makao makuu madogo ya polisi Dar es Salaam,kitengo cha Ukaguzi wa Silaha na milipuko,ameiambia mahakama kuwa,mnamo Novemba 25,mwaka 2020,askari aliyemtaja kwa jina la Goodluck,kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa makosa ya jinai (DCI)alimkabidhi Bastola moja na risasi tatu, inayodaiwa kutumiwa na Mshtakiwa Adam Kasekwa,yenye namba A5340,iliyosajiliwa mwaka 1995.

Koplo Hafidh ameendelea kusema,baada ya kukabidhiwa bastola hiyo,alianza uchunguzi mara moja,ambapo alitumia risasi mbili kati ya tatu alizokadhiwa kujaribu na kujirisha kuwa ilikuwa inafanya kazi.Alimaliza uchunguzi wake Novemba 26 na kuikabidhi bastola hiyo pamoja na taarifa ya uchunguzi kwa Afande Swila,ofisi za Mkurugenzi wa Makosa ya jinai Novemba 27.

Shahidi huyo poa amewakilisha mahakamani vielelezo vinne vya ushahidi wake,ambavyo ni taarifa ya ukaguzi,bastola,maganda mawili ya risasi,pamoja na risasi moja.