Na Leo Mapuli.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,kwa mara nyingine imelazimika kuahiririsha kesi ya Ugaid inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe,na wenzake watatu,hadi Agosti 27.
Katika kesi hiyo,Mbowe na wenzake walipaswa kuletwa mahakamani hapo leo Agosti 13,kwa ajili ya shauri lao kusomwa tena,lakini hawakuweza kufika kwa sababu mbalimbali zilizoelezwa mahakamani hapo,ikiwemo tatizo la usafiri kutoka gerezani hadi mahakamani.
Baada ya watuhumiwa kushindwa kuletwa mahakamani,Mahakama ililazimika kusikiliza kesi kesi hiyo kwa njia ya Video,ambapo hata hivyo zoezi likaingiwa dosari baada ya watuhumiwa wote kushindwa kuunganishwa Pamoja ili kufuatilia kesi hiyo kutokana kuwa katika magereza mawili tofauti.

Kufuatia hali hiyo,Mahakama imepanga kusikiliza tena kesi hiyo Agosti 27,ambapo upande wa utetezi umeiomba Mahakama kuwaleta watuhumiwa mahakamani hapo na si kusikiliza kesi kwa njia ya Video ambayo kwa mara ya pili imeshindwa kufanya kazi kwa sababu mbalimbali.
Katika hatua nyingine,upande wa utetezi umewasilisha taarifa mahakamani hapo ya kusudio la kuiomba Mahakama ipeleke Mahakama Kuu kama suala la kikatiba,matamshi yanayodaiwa kutolewa na “Taasisi” moja ya juu ya serikali yenye kuleta mashaka ya kesi hiyo kuingiliwa.
“Kuna Taasisi fulani hapa nchini,sina haja ya kuitaja,watu wote wanaifahamu,wameisikia,tunachosema taasisi ile kwa maneno iliyoyatoa,kwa maoni yetu sisi na wateja wetu,yameingilia moja kwa moja uhuru wa Mahakama,siyo Mahakama hii tu ila ni Pamoja na Mahakama ambayo itakayokwenda kusikiliza shauri la kigaidi (Mahakama Kuu),na kwa kuwa Mamlaka ile ni Mamlaka yenye nguvu na ushawishi,basi matamshi yale yaliyotamkwa,yamewafanya wateja wetu waone kuwa tayari wameshahukumiwa,na hakuna namna nyingine wanaweza wakapata Fair Trial”,amesema Peter Peter Kibatala,wakili anayemtetea Mbowe na wenzake,alipozungumza na wandishi wa Habari nje ya mahakama baada ya kesi kuahirishwa.
Mbowe, pamoja na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka ya ugaidimyanayopingwa vikali na wafuasi wa CHADEMA wanaodai kuwa ni matokeo ya vuguvugu la kudai katiba mpya lililokuwa limeanzaa kushika kasi katika maeneo mbalimbali ya nchi chini ya CHADEMA na vyama vingine vya siasa Pamoja na Wanaharakati wa masuala ya Haki nchini Tanzania.
Kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo itatajwa tena Mahakamani hapo Agosti 27,na kwa mara ya kwanza,imehudhuriwa na ujumbe wa kimataifa akiwemo Balozi wa Sweden,Umoja wa Ulaya na Ujumbe kutoka jumuia ya Afrika Mashariki.
Habari Zaidi
GENGE LA VIJANA WA KISUKUMA KATAVI LAFUMWA LIKIFANYA “CHAGULAGA”.
AFRICAN COURT ON HUMAN AND PEOPLES’ RIGHTS DELIVERED 14 JUDGMENTS
KESI YA MBOWE:SHAHIDI WA TATU (JAMHURI) AANZA KUTOA USHAHIDI.