February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

KESI NDOGO YAIBUKA TENA KWENYE KESI YA MBOWE NA WENZAKE

Na Antony Rwekaza

Kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi namba 16/2021 inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake imeibuka kufuatia Mahakamani kupokea mapingamizi mawili yaliyowekwa na mawakili wa upande wa utetezi, wakidai maelezo yanayodiwa kuwa ya mshtakiwa namba tatu Mohamed Ling’wenya yalichukuliwa baada ya mshitakiwa kulazimishwa.

Mawakili wa Jamhuri wameomba kupewa muda wa kujiandaa kwa ajili ya kuaza kusikiliza kesi hiyo ndogo, upande wa utetezi umekubali na Jaji ameiahirisha kesi hiyo mpaka kesho Novemba 10, 2021 saa 5:00 asubuhi.

Ikumbukwe leo shahidi wa nane upande wa Jamhuri alikuwa akiendelea na ushahidi wake hivyo ataendelea anatarajiwa kuendelea na kukamilisha ushahidi baada ya kesi ndogo kukamilika ambayo nayo itajumuisha mashahidi kutoka pande zote, lakini upande wa Jamhuri ndiyo unaotarajiwa kuanza.