February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

KENYA : WATANGAZA ZAWADI NONO YA MILIONI 60 KWA ATAKAYETOA TAARIFA KUHUSU WASHUKIWA WA UGAIDI

Idara ya upelelezi wa Jinai –(DCI), nchini kenya imeanzisha msako dhidi ya washukiwa watatu wa ugaidi ambao walitoroka gereza kuu la Kamiti Jumatatu asubuhi.

Kulingana na DCI, watatu hao, kwa majina Musharaf Abdalla, Mohamed Ali Abikar na Joseph Juma Odhiambo walitoroka kutoka gereza hilo mwendo wa saa saba usiku.

Haijabainika wazi jinsi ambavyo watatu hao walifanikiwa kutoka kwenye gereza hilo ambako kuna ulinzi mkali, hata hivyo Zawadi ya shilingi milioni- 60 imetangazwa kwa yeyote atakayetoa habari za kuwezesha kukamatwa kwa watatu hao.

Mshukiwa wa pili Mohamed Ali Abikar alikamatwa kufuatia kujihusisha kwake katika shambulizi ya kigaidi kwenye chuo kikuu cha Garissa mnamo tarehe 2 April mwaka 2015.

Mshukiwa wa tatu Joseph Juma Odhiambo alikamatwa tarehe 21 Novemba mwaka 2019 katika eneo la Bulla Hawa nchini Somalia, akiwa anajaribu kujisajili kwenye kundi la Al-Shabaab.

DCI inasema kuwa Habari zozote kuwahusu watatu hao zitahifadhiwa kwa siri.