March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

KENYA: WANJIGI AACHILIWA HURU


Mahakama nchini Kenya imelazimika kumuachilia huru mfanyibiashara Jimi Wanjigi baada ya kubaini kulikuwepo na agizo la mahakama kuu nchini humo la kuzuia ukamataji wake.


Wanjigi alikamatwa hapo jana na Kitengo cha Polisi cha kupambana na ugaidi kwa madai ya kujipatia ardhi kwa njia ya udanganyifu.


Hata hivyo mawakili wake waliiambia mahakama kuwa polisi hao walisababisha hasara ya kiasi cha zaidi ya Milioni 10 za Kenya baada ya kuvamia kwa nguvu na kuharibu mali katika ofisi za Wanjigi walipokwenda kumkamata.


Wanjigi aliyekuwa akiwania tiketi ya urais na chama cha ODM, amedai masaibu yake yanachangiwa na kinara Raila Odinga aliyewahi kuwa mwandani wake.