December 4, 2022

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

KENYA: ODINGA AMTEUA MARTHA KARUA KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS

Raila Odinga akiwa na Martha Karua

Kiongozi wa Azimio la Umoja,Raila Odinga amemteua Kiongozi wa Chama cha NARC  ,Martha Karua kuwa mgombea mwenza katika uchaguzi mkuu unatorajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Odinga amesema bidii na rekodi ya haki za binadamu ya Kariua ndivyo vilivyochagiza uteuzi huo baada ya kushauriana kwa kina na kufikia maamuzi hayo akisema Ofisi ya naibu wa Rais ni ofisi ambayo haiwezi kushindana na ofisi ya Rais hivyo atakayeshikilia wadhifa huo lazima awe mfanyakazi mwenza.

Endapo Karua atachaguliwa mwezi Agosti kuwa Makamu wa Rais ataandika historia ya kuwa  mwanamke wa kwanza nchini Kenya kushikilia wadhifa huo.

Karua si mgeni katika siasa za nchini Kenya amewahi kushikilia nafasi za Uwaziri na hata kusimamia sekta mbalimbali kwa takribani miaka sita na pia ni miongoni mwa wagombea 11 waliofanyiwa mchujo.