Mahakama Kuu jijini Nairobi,Kenya imeahirisha kusikiliza shauri la Mfanyabiashara Jimi Wanjigi ili kutoa muda wa kuthibitishwa kwa hati ya kuzuia kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo mpaka Februari 9,2022.
Wanjgi alifikishwa mahakamani hii leo baada ya kukamatwa hapo jana na maafisa wa polisi katika ofisi zake zilizopo Kwacha jijini Nairobi kwa madai ya kujipatia ardhi kwa njia ya udanganyifu.na awali alikataa kujitokeza mahakamani akidai ana hati ya kuzuia ukamataji wake.

Timu ya mawakili wanaomuwakilisha Wanjigi wakiongozwa na Willis Otieno walimueleza Hakimu Mwandamizi Benard Ochoi kuwa walipata hati ya kuzuia ukamataji mnamo tarehe 8,Januari majira ya saa tisa unusu jioni hivyo Mahakama iliahirisha kesi hiyo kwa muda ili kuweza kujiridhisha na kuamua kama Wanjigi atasomewa mashitaka yake hii leo.
Aidha Wakili Otieno ameieleza mahakama hiyo kuwa Maafisa wa polisi Kutoka kitengo cha kupamnbana na ugaidi wameharibu mali zenye thamani ya Zaidi ya Shilingi za Kenya Milioni kumi wakati walipovamia ofisi za Wanjigi na kuharibu vifaa nab ado wanaendelea kufanya tathimini ili kutoa gharama sahihi.
Habari Zaidi
ETHIOPIA: AJIUNGA CHUO KIKUU AKIWA NA MIAKA 69
MWANDAAJI MISS RWANDA KUFUNGULIWA MASHITAKA YA UHALIFU WA KINGONO
KENYA: ODINGA AMTEUA MARTHA KARUA KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS