February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

KENYA: DAKTARI ALIYEUA WATOTO WAKE AFARIKI DUNIA


Daktari aliyefahamika kwa jina la James Gakara,ambaye anadaiwa kuwauwa watoto wake wawili na kisha yeye mwenyewe kufanya jaribio la kujitoa uhai amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Nakuru nchini humo.


Gakara kabla ya kifo chake alikuwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum ( ICU) tangu alilopatikana hana ufahamu nyumbani kwake na anatuhumiwa kwa kuwauwa watoto wake wenye umri wa miaka 3 na 5.Kwa mujibu wa maafisa wa polisi anadaiwa kuwachoma sindano ya sumu watoto hao na pia kisu kilikutwa katika eneo la tukio.

Watoto hao walikutwa wamefariki huku povu zito likiwa linatoka midomoni mwao wakati Datari huyo alikutwa amelala kitandani akiwa hajitambui na alikimbizwa katika Hospitali ya Nakuru kupatiwa matibabu wakati akisubiriwa kuhojiwa na kushitakiwa kwa kesi ya mauaji.

Majirani walipata wasiwasi baada ya kuona Daktari amejifungia ndani na watoto kitendo ambacho hakikuwa cha kawaida na kutoa taarifa polisi.

Familia ya Dkt Gakara imeeleza kuwa Gakara alikuwa akiwapenda watoto wake na suala hilo limewaacha wakiwa na majonzi, na kueleza kuwa ndugu yao hakuenyesha dalili zozote za kuwa na msongo wa mawazo.

Chama cha Madaktari nchini Kenya kimesema afya ya akili ya madaktari inapaswa kupewa kipaumbele.