Mwanamume mmoja nchini Kenya ambaye ni dereva,David Musyoka amejikuta matatani baada ya kung’atwa na nyoka aliyedai kuwa amedondoka kutoka angani.
Kwa mujibu wa Musyoka (39) anasema nyoka huyo aliangushwa na ndege aina ya tai juu ya gari alilokuwa akiendesha na nyoka huyo alitambaa na kuingia kwenye gari kupitia dirishani na kisha kumuuma kwenye mkono.
Baada ya tukio hilo Musyoka alilazwa hospitali katika wodi ya upasuaji siku ya jumatatu na kwa mujibu wa taarifa aliondoka hospitali hapo jana.
Tukio hilo la kushangaza limewaacha midomo wazi watu mbalimbali huku wengine wakimuita nyoka huyo kuwa ni shetani.
Chanzo BBC
Habari Zaidi
ETHIOPIA: AJIUNGA CHUO KIKUU AKIWA NA MIAKA 69
MWANDAAJI MISS RWANDA KUFUNGULIWA MASHITAKA YA UHALIFU WA KINGONO
KENYA: ODINGA AMTEUA MARTHA KARUA KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS