February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

KAULI ZA WAKUU WA MIKOA WATANO KWENYE MAJIJI, KITENDAWILI

Zifutazo ni baadhi ya nukuu za Wakuu wa Mikoa watano ambao wanaongoza majiji, wakielekeza wananchi kuchukua tahadhari juu ya mlipuko wa tatu wa janga la Corona.

  • “Ni lazima kuvaa barakoa unapoingia kwenye chombo cha usafiri, kuwepo na vitakasa mikono huduma hiyo kwa wamiliki wa mabasi, kila katika basi kunakuwa na ‘level seat’, usimamizi upo, LATRA wapo MA-RTO wapo wa kusimamia hili jambo” Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala
RC Dar es Salaam, Amos Makala
  • “Mganga Mkuu wa Mkoa amesema kuwa wanaokwenda kumuona mgonjwa wasizidi watu watatu, sisi wa mkoa tumeyapokea lakini nyongeza yake ni ukitaka kwenda kumuona mgonjwa, kumpelekea chakula bila kuvaa barakoa hatutakuruhusu, ili uruhusiwe kumuona kwenye zahanati, kituo cha afya, hospitali ya serikali au ya binafsi tunawaomba mvae barakoa kwa faida yako na mgonjwa pia,” amesema Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka.

-“chukueni tahadhari achana na mikusanyiko isiyo ya halali na kutumia barakoa, kunawa  maji tililika kujikinga ili kujikinga na ugonjwa wa korona, ambao unasumbua dunia katika kipindi hiki” Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela

RC Arusha, John Mongela
  • “Hatuwezi kukataza watu kwenda sokoni na kwenye shughuli zingine za kiuchumi zinazokusanya wengi; tunachosisitiza ni kwamba kila anayeenda kwenye kusanyiko azingatie kanuni ya kujilinda na kuwalinda wengine; vyombo vua habari saidieni katika eneo hilo” Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Robert Gabriel
Rc Mwanza, Robert Gabriel

-“Jamani ninapofikia kutoa maagizo na tamko naomba wananchi mchukue tahadhari na usimamizi ufuatwe kwa mujibu wa maelekezo na watoto wenye umri chini ya miaka 18 watapewa maelekezo namna ya kujikinga,”amesema Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera

Kauli hizo zimechagizwa zaidi na maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Afya Mendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Gwajima kusema vongozi watawajibishwa endapo watashindwa kuwajibika kwenye mapambano dhidi ya janga la Corona

-“Napenda kuweka wazi kuwa, serikali haitaendelea kuvumilia kuona baadhi ya viongozi hawatimizi wajibu wao kwenye kusimamia mapambano dhidi ya UVIKO-19 ” Waziri wa Mendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima

Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima

Majiji hayo ya Dar es Salaam,Dodoma, Mwanza, Arusha na Mbeya ni kati ya sehemu zenye harakati ya mikusanyiko ya watu wengi, kutokana na idadi kubwa ya watu waliyopo kwenye sehemu za mijini kutokana na kuwepo kwa shughuli nyingi za kiuchumi.

Kitendawili ni kuwa kauli hizo zitafanikiwa kwa kiwango gani na kwa njia rafiki ambazo zitaweza kuepuka maambukizi mapya bila kuvunja haki za binadamu?

Watetezi TV ikiwa inafatilia kwa kina utekelezwaji na mapokeo ya kauli hizo kwa wananchi wa maeneo hayo, inawataka wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari muhimu zinazotolewa na wataalamu wa afya ili kuepuka ongezeko la maambukizi mapya ya Corona.