December 4, 2022

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

KAMATI MAALUM YASHAURI CHANJO YA COVID-19 ITOLEWE

Kamati Maalum ya tathimini kuhusu ugonjwa wa Covid-19 iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeishauri serikali kuendelea na hatua za kuruhusu matumizi huru ya chanjo dhidi ya Covid-19 kwa kutumia chanjo ambazo zimeorodheshwa na WHO kwani chanjo hizo ni salama kisayansi.

Kamati hiyo imetoa mapendekezo yao hii leo Mei 17,wakati ilipowasilisha ripoti hiyo kwa Rais Ikulu jijini Dar es salaam na kutoa wito kwa wananchi kupewa fursa ya kuamua kuchanja au la

“Kipaumbele cha utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 nchini kwa kuanzia kiwe katika makundi muhimu ikiwemo
Wahudumu katika vituo vya kutolea huduma za afya na watumishi walio katika mstari wa mbele wa utoaji wahuduma mathalani watumishi sekta ya utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini na mahujaji,Wazee na watu wazima kuanzia umri wa miaka zaidi ya 50,Watu wazima wenye maradhi sugu mengine mathalani kisukari, shinikizo la damu,maradhi ya mfumo wa upumuaji, magonjwa ya figo n.k,Watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na Wasafiri wanaokwenda nje ya nchi,”amesema Prof Said Aboud wakati akiwasilisha ripoti hiyo.

Aidha Kamati imeitaka serikali  itoe taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa wa COVID-19 na ichukue hatua madhubuti kuimarisha hatua zote za afua za kinga (interventions) katika ngazi zote ili kuepusha wimbi la tatu la ugonjwa
huo.

“Serikali iendelee kuhakikisha matumizi ya tiba asili na tiba mbadala katika mfumo rasmi wa tiba za kisasa yanazingatia misingi ya kisayansi” ameongeza

Tangu kutokea kwa mlipuko wa janga la virusi vya corona serikali nyingi duniani zimeweka shuruti la kutotoka nje (lockdown) kwa raia wake ili kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo,Kamati Maalum ya Kutathimini Covid-19 nchini imeiomba serikali kuangalia mazingira ya Kitanzania katika udhibiti wa janga hilo katika kuamua kuweka au kutoweka ‘lockdown’ ili kuruhusu ukuaji wa uchumi.