March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

JUHUDI ZA KUMPATA MAKONDA ZAGONGA MWAMBA, HAKIMU ATOA ODA YA KUSAKWA KILA KONA

Na: Anthony Rwekaza

Mleta maombi kwenye shauri namba 1/2022 mwandishi wa habari ambaye aliyewai kuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Said Kubenea akiwakilishwa na mawakili wake leo Februari 8, 2022 wameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kutoa hati za wito (samoncor) wa kumtafuta Pual Makonda kwenye maeneo saba ikiwemo nyumbani anapozaliwa Kijiji cha Koromijee na kwenye magazeti ikiwa ni baada ya juhudi za kumpata kushindikana.

Maeneo saba ambayo wameomba kupelekea hati za wito ni ofsi ya ambayo Makonda alikuwa anafanyia kazi ambayo ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Nyumba aliyokuwa anaishi mara ya mwisho eneo la Masaki Dar es salaam, Orzone Pharmacy eneo ambalo linadaiwa uwa anapenda sana kutembelea, Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, Bandarini Dar es salaam, eneo anapozaliwa Kijiji cha Koromijee Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza na kwenye magazeti.

Kati ya maeneo hayo waliyoomba, Hakimu amekubali kutoa hati ya wito huo kwa ajili ya kupelekwa kwenye maeneo matatu, ambayo ni makazi yake alipokuwa anaishi mara ya mwisho, Kijijini Koromijee na kwenye magazeti ili kufanya taarifa zimfikie popote pale atakapokuwa ili kufika Mahakamani.

Aidha Wakili Daines Makala anayewakilisha upande wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI pamoja Mwendesha mashtaka Mkuu wa Serikali DPP, amesema yeye hawezi kujibu hoja ilivyowasilishwa na na waleta maombi juu ya mjibu maombi namba tatu kwa kuwa hamuwakilishi, ambapo kwa niaba ya DPP na DCI ameomba kupewa muda kwa ajili ya kujibu maombi.

Kutokana na mawakili wa mleta maombi wakiongozwa na Wakili Kicheere Nyaronyo kutokuwa na pingamizi juu ya ombi hilo Hakimu Mkazi Aron Lyamuya anayesikiliza shauri hilo ameliahirisha mpaka March 2, 2022 ambapo litatajwa kwa mara nyingine.

Shauri hilo limefunguliwa na Saidi Kubenea ambaye ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Ubungo, aliwasilisha maombi Mahakamani ili kuruhusiwa kumshtaki Paul Makonda, akidai kuwa hatua hiyo ni kufuatia Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kushindwa kutimza jukumu lao ipasavyo kwa kumfungulia mashtaka Paul Makonda baada ya tukio wanalodai kuwa alivamia kituo cha Runinga Clouds TV.

Awali Wakili wa Kubenea amesema wamefanya kila jitiada ya kumpata Makonda ambaye aliwai kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam lakini zimeshindikana, ambapo ameieleza Mahakama kuwa walimtafuta maeneo mbalimbali ikiwemo alipokuwa anaishi akiwa Mkuu wa Mkoa eneo la Masaki lakini walikuta ameshahama, sehemu nyingine ambazo wamedai kumtafuta ni kwenye maeneo ambayo upenda kutembelea pamoja na kumtafuta kwa njia ya simu lakini hata hivyo hawakufanikiwa.