March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

JESHI LA MALI LAWAACHILIA HURU RAIS NA WAZIRI MKUU

Viongozi wa mapinduzi nchini Mali wamewaachilia huru Rais wa mpito Bah N’daw na Waziri Mkuu wake Moctar Ouane waliokuwa wanazuiliwa katika kambi ya kijeshi tangu jumatatu.

Viongozi hao ambao wamelazimishwa kujiuzulu nafasi zao na kuvuliwa madaraka na jeshi kwa kile Kiongozi wa Mageuzi hayo , Kanal Goïta alichodai kuwa amewafuta kazi baada ya kuunda serikali mpya bila kushauriana naye wakati ni makamu wa rais anayesimamia masuala ya usalama.

Goita alijitangaza kuwa Rais wa mpito baada ya mapinduzi hayo ikiwa ni mapinduzi ya pili kuyafanya katika kipindi cha mwaka mmoja