February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

JESHI LA MALI LANDELEA KUMSHIKILIA RAIS NA WAZIRI MKUU KAMBINI

Rais wa Mali Bah Ndaw kabla ya kutekwa.

Jeshi la Mali linaendelea kuwashikilia rais wa nchi hiyo Bah Ndaw,Waziri Mkuu Moctar Ouane pamoja na waziri wa ulinzi Souleymane Doucore katika kambi moja ya jeshi  tangu mapinduzi ya jumatatu baada ya rais huyo kutangaza  baraza jipya la mawaziri lilooacha kujumuisha viongozi wa kijeshi walioshiriki katika mapinduzi ya mwezi August mwaka jana yaliyomuondosha madarakani rais wa kipindi hicho,Ibrahim Boubacar Keita.

Umoja wa Mataifa na umoja wa Afrika vimeshutumu vibaya kitendo hicho na kutoa rai waachiliwe huru ili kuondoa sintofahamu iliyotawala katika taifa hilo masikini.

Ujumbe maalumu kutoka ECOWAS unataraji kufanya ziara katika mji mkuu wa Mali Bamako kujaribu kushawishi kuachiliwa huru kwa viongozi hao.

Kinara wa Mapinduzi hayo Assimi Goita ambae aliteuliwa kushika wadhifa wa Makamu wa ameshutumu viongozi hao kuwaondosha katika serikali maafisa muhimu wa Jeshi Sadio Camara na Colonel Modibo Kone walioshiriki kumpundia Keita lakini wamepewa majukumu mwengine ya kusimamia masuala ya usalama nje ya serikali ya kiraia.