March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

JACKLINE MENGI AAMBULIA PATUPU MIRATHI YA MZEE MENGI

Na Leonard Mapuli/Paul Kisabo, Dar es Salaam.

Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ya Dar es Salaam imetoa uamuzi kuwa watoto wa Marehemu Reginald Mengi;-Abdiel na Benjamin Mengi kuwa wasimamizi wa mirathi ya mali alizoacha marehemu baba yao (Reginald Mengi). Katika uamuzi huo, mahakama imeagiza usimamizi na mgawanyo wa mirathi uanze mara moja. Akisoma hukumu hiyo yenye kurasa 72 mnamo Mei 18/2021 Jaji Mlyambina alisema kuwa wosia wa mwisho wa Marehemu Dkt. Mengi ulioandikwa Agosti 17,2017 haukuzingatia misingi ya kisheria ya uandishi wa wosia. Katika shauri hilo watoto wa marehemu Dkt. Mengi walikuwa wakipinga wosia uliodaiwa kuachwa na Marehemu baba yao kwa madai kwamba wosia huo haukufungwa ‘sealed’ na saini iliyopo kwenye wosia huo ni tofauti na sahihi zingine za Marehemu na pia kwa wakati huo baba yao hakuwa na uwezo wa kuandika kutokana na matatizo makubwa ya kiafya aliyokuwa nayo tangu mwaka 2016.Aidha watoto hao walidai kuwa wosia uliwabagua na urithi wote aliachiwa mkewe mpya na watoto mapacha na hivyo wosia huo ulikuwa kinyume na sheria sababu uliwabagua watoto bila sababu za msingi na za kisheria.