February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

IRINGA: MWANACHUO ADAIWA KUNYONGWA NA MPENZIWE

Jeshi la polisi mkoani Iringa linamshikilia mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa, Prudence Patrick (21) kwa tuhuma za kumnyonga hadi kufa mpenzi wakeambaye ni mwanafunzi mwaka wa kwanza chuoni hapo,Petronel Mwanisawa (22).

Kamanda wa Polisi Iringa,Juma Bwire amesema wamemkamata mtuhumiwa akiwa katika kituo kikuu cha mabasi Iringa akiwa anatoroka kuelekea nyumbani kwao Bukoba mkoani Kagera.

Chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi na mtuhumiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo alituma ujumbe mfupi kwa mama wa Marehemu na kumtaarifu kuwa Petronila amefariki.

Tukio hilo limetokea Juni mosi mwaka huu na mwili wa Marehemu unaagwa hii leo chuoni hapo na kisha utasafirishwa kuelekea Sumbawanga kwa mazishi.