February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

IRELAND KUMTIMUA BALOZI WA ISRAEL

KIKAO CHA KUIADHIBU ISRAEL:Wabunge wa Ireland wakiwa wamevalia barakoa zenye nembo za Palestina ikiwa ni ishara ya umoja wao na nchi hiyo.

Na Leonard Mapuli

Nchi ya Ireland inaandaa  mpango wa kupiga kura juu ya mabadiliko ya dharura  ambayo kama yatapaitishwa yatairuhusu nchi hiyo kumfukuza balozi wa Israel nchini humo na kuiwekea Israel  vikwazo mbalimbali vikiwemo vya uchumi.

Hatua hii ni kuunga mkono baadhi ya nchi za Ulaya zilizolaani hatua ya Israel kuishambulia Palestina na kuua watu zaidi ya 200 wakiwemo watoto wakati Israel ilipopambana na wapiganaji wa Hamas wanaoukalia mji wa Gaza.

Serikali ya Ireland inaunga  mkono hatua ya bunge lake kujadili juu ya hatua hiyo inayolipa  bunge nguvu ya kuamua hatua ama adhabu yoyote kwa nchi nyingineinayokiuka haki za binadamu  bila hata kuipa muda wa kujitetea  dhidi ya tuhuma, maarufu kwa jina la “De facto annexation”. Mamlaka za Israel zinadaiwa kuivamia ardhi ya Palestina na Umoja wa Ulaya pia uliishutumu Israel kwa hatua hiyo.

Kwa Mujibu wa Waziri wa mambo ya Nje wa Ireland Simon Coveney, Ombi la Israel kuwekewa vikwazo na Ireland liliwasilishwa bungeni na chama cha upinzani  cha Sinn Fein kwa madai kuwa hatua hiyo itakuwa muhimu na heshima juu ya hisia waliozoonesha raia wa Ireland wakati  Palestina iliposhambuliwa na Israel majuma mawili yaliyopita.

Mbali na kufukuzwa kwa balozi wa Israel nchini Irelend (Endapo sheria hiyo itapita) hatua hiyo pia itaambatana na kuharibika kwa diplomasia baina ya nchi hizo mbili pamoja na vikwazo katika medani za siasa na kijamii.

Waziri Coveney aliyewakilisha Ireland katika Kikao cha baraza la usalama la umoja wa mataifa majuma kadhaa yaliyopita alisisitiza pia kuwa baraza hilo halitakiwi kukifumbia macho kikundi cha wapiganaji wa Hamas walioishambulia  Israel kwa maroketi kabla ya azimio la kuisaidia Palestina kufikiwa na umoja huo.

Hatua ya kuiwekea vikwazo Israel imekuja siku chache baada ya kukoma kwa mapigano makali ya siku 11 kushuhudiwa kwa miaka ya karibuni yaliyouathiri zaidi mji wa Dublin nchini Palestina.