March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

INDIA : WANNE MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA KENGE

Wanaume wanne nchini India wanaodaiwa kuwa wawindaji wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka Kenge kwa zamu katika mbuga ya Sahydari Tiger huko Maharashthra na kujirekodi.

Inaelezwa kuwa tukio hilo lilibainika baada ya simu ya mmja wa wanaume hao kukutwa na video zinazoonyesha wakiwa wanatekeleza tukio hilo la kustaajabisha.

Video za CCTV ziliwaonyesha wanaume hao walionekana karibu na kuingia katika mbuga hiyo mara kadhaa hali iliyosababisha kutiliwa mashaka na Mamlaka ya hifadhi hiyo.

Aidha licha ya video hiyo iliyoonyesha wakimbaka Kenge maofisa wa polisi wamekuta pia picha za wanyama wengine kama Kulungu katika simu za wanaume hao.

Kenge huyo aliyebakwa kwa kitaalamu Bengal Tigers ni miongoni mwa viumbe wanaolindwa sana nchini humo kwani wapo hatarini kupotea,na iwapo wanaume hao watakutwa na hatia watakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 7 gerezani.