December 4, 2022

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

IJUE SHERIA YA KUZUIA UGAIDI TANZANIA

Na Antony Benedicto

Sheria ya kuzuia Ugaidi Nchini Tanzania ya mwaka 2002(Prevention Of Terrorism Act), imeeleza tafsiri ya makosa ya Ugaidi na adhabu zake, kwenye picha ni kifungu cha 18(1) kinachoelezea aina ya kosa na adhabu kwa mtuhumiwa atakayebainika na hatia mbele ya mahakama “kifungo kisichopungua miaka 20 na kisichozidi miaka 30”

Sheria hiyo inaundwa na vifungu 54 ambavyo vimegawanyika katika sehemu tofauti, kuanzia hatua ya awali ya kuzuia ugaidi, kutuhumu, uchunguzi, mpaka hatua ya mwisho ya kumchukulia mtuhumiwa au watuhumiwa ambao ubainika kuwa wametenda makosa yanayokiuka sheria hiyo.

Ikumbukwe Jeshi la Polisi Nchini Tanzania jana alihamsi Julai 22, lilitoa taarifa kwa umma kuwa linamshikiria Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe kwa uchunguzi wa tuhuma za Ugaidi.