Mataifa ya Marekani na Ubelgiji yamepinga hukumu ya kifungo cha miaka 25 gerezani iliyotolewa na mahakama ya Rwanda dhidi ya Paul Rusesabagina zikisema wakidai Rugesabina hakupewa haki ya kisheria.
Hata hivyo Rwanda imesema madai hayo yaliyotolewa na Ubelgiji kuwa ni dharau na hivyo imesitisha mkutano wa kando uliokuwa ufanyike Newyork Marekani uliotarajiwa kuzikutanisha pande hizo mbili.
Naibu Waziri Mkuu wa Ubelgiji na waziri wa mambo ya nje, Sophie Wilmès alisema kuwa alipata taarifa kuwa hukumu ya Rusesabagina imetolewa mjini Kigali na kuwa Kuanzia mwanzo wa kesi hiyo japokuwa Ubelgiji ilikuwa ikiendelea kuomba masuala kadhaa yafanyike, inaonyesha kuwa kesi ya Rusesabagina haikuendeshwa mahakamani kwa njia iliyo ya uwazi na haki kisheria hasa haki yake ya kujitetea.
Rusesabagina (67) ambaye ni mzaliwa wa Rwanda pia ana uraia wa Ubelgiji na ana kibali cha Marekani amehukumiwa miaka 25 gerezani baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki katika vitendo vya ugaidi, Rusesabagina alituhumiwa kuwa mwanzilishi na mfadhili wa kundi moja la waasi ambalo lilitekeleza mashambulio nchini Rwanda mwaka 2018 na kuwaua watu tisa.
Habari Zaidi
ETHIOPIA: AJIUNGA CHUO KIKUU AKIWA NA MIAKA 69
MWANDAAJI MISS RWANDA KUFUNGULIWA MASHITAKA YA UHALIFU WA KINGONO
KENYA: ODINGA AMTEUA MARTHA KARUA KUWA MGOMBEA MWENZA WA URAIS