Na: Anthony Rwekaza
Hukumu ya Kesi namba 220/2018 ya madai ya fidia ya ya Bilioni 10 iliyofunguliwa na Mwanasiasa Benard Membe dhidi ya Mwanaharakati Cyprian Msiba na wenzake, imesogezwa mbele ambapo imepangwa kutolewa hukumu Oktoba 28, 2021 kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam.
Hatua hiyo imekuja kufuatia taratibu za maamuzi ya hukumu kushindwa kukamilika kufikia leo Jumanne Oktoba 12, 2021 siku ambayo ilipangwa kutolewa Hukumu ya kesi hiyo.
Katika Shauri hilo la madai Membe alimshitaki Musiba kwa kuidai kumtuhumu bila uthibitisho kuwa alikuwa anahujumu harakati za hayati Rais Magufuli kwaletea maendeleo wananchi huku akidai kuwa mbinu mojawapo ni kufanya hujuma kuelekea maandalizi ya Uchaguzi Mkuu 2020 kwenye hatua za awali za kupitisha Mgombea wa nafasi hiyo alitakiwa kuwakilisha Chama cha Mapinduzi CCM.
Mwanaharakati huyo katika kesi hiyo anashtakiwa kwa kumtuhumu Membe kuwa anamhujumu Rais John Magufuli asitekeleze majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo huku akidai kwamba mbinu mojawapo ya kukamilisha hujuma hizo ni maandalizi anayofanya kugombea urais mwaka 2020 kupitia CCM.

Kesi hiyo iliyofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam Mwaka 2018 na kuanza kusikilizwa kwa mara ya kwanza February 26,2021 mbele Jaji Joaquine De Mello , huku Membe akiwakilishwa na Wakili wake Jonathan Mndeme, awali upande wa utetezi uliweka mapingamizi matatu lakini Desemba 27, 2019 mapingamizi yote yalitupiliwa mbalimbali kutoka kilichodaiwa kuwa hayakukidhi matakwa ya kisheria.
Msiba ambaye alijitamburisha kama ‘Mwaharakati huru’ akidai kumtetea aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli na Serikali ya awamu ya tano, alikuwa pia akitumia vyombo vyake vya habari kuelezea mambo aliyodai yanafanywa na Serikali hiyo iliyokuwa madarakani, hivyo Membe alidai kuchafuliwa kupitia vyombo hivyo, hatua iliyopelekea na aliyekuwa Mhariri na watendaji wengine wa vyombo hivyo ‘Gazeti la Tanzanite’ kujumuhishwa pamoja na Msiba kwenye kesi hiyo.
Membe ambaye aliwai kuwa Waziri wa Mambo Nje katika Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Msataafu Jakaya Mrisho Kikwete, na kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu 2020, kupitia tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo amekuwa akifika Mahakamani kusikiliza kesi hiyo akiwa sambamba na Wanasheria wake.
Kwenye Kesi hiyo Mwanasiasa huyo Benard Membe anadai fidia ya kiasi cha Shilingi Bilioni 10 kutokana madai ya jina lake kuchafuliwa na alichodai kuwa ni kashfa dhidi yake.
Habari Zaidi
KIKOSI KAZI KITASAIDIA KULETA MARIDHIANO – JK
NI MIAKA MITANO SASA TOKEA LISSU ASHAMBULIWE
SHAHIDI JAMHURI AELEZA KINA MBOWE WALIVYOSUKA MPANGO WA KUTENDA UGAIDI