February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

HEZROG RAIS MPYA ISRAEL

Mwanasiasa wa muda mrefu nchini Israel, Isaac Herzog wa  chama cha Labour amechaguliwa kuwa rais wa taifa hilo.Hezrog anakuwa rais wa 11 wa wa Israel na atashika madaraka rasmi Julai 2 mwaka huu.

Hezrog amepata kura za wabunge wenge kwa kupata kura 87 kati ya kura 120 za wabunge wanaounda Bunge la Knesset huku mpinzani wake Miriam Peretz akipata kura 33.

Rais huyo mpya anatajwa kuwa ni mwanasiasa mzoefu ni mtoto wa Chaim Hezrog ambaye alikuwa Rais wa Israel mwaka 1983-1993, Isaac pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Labour, na aliwahi kuwa kiongozi wa upinzani  na katika kipindi cha karibuni aliongoza idara ya uhamiaji nchini humo.