February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

HAYA NDIYO MASHITAKA YANAYOMKABILI MBOWE

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Freeman Mbowe pamoja na wenzake watatu hapo jana Julai 26/2021 walifikishwa katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka matano.

Kwsi hiyo ya uhujumu uchumi namba 63/2020 iliyofunguliwa na Mwendesha mashitaka wa serikali dhidi ya Halfani Bwire Hassan,Adam Hassan Kasekwa,Mohamed Abdilah Lingwenya na Freeman Mbowe.

Katika shitaka la kwanza watuhumiwa wanashitakiwa kwa madai ya kupanga njama za kulipua vituo vya mafuta pamoja na sehemu zenye mikusanyiko ya watu wengi kitendo ambacho kinatishia usalama wa wananchi na kudhamiria kutishia umma wa watanzania; watuhumiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Mwezi Mei mosi na Agosti 1,2020 katika hoteli ya Aishi iliyopo Wilayani Moshi na maeneo mengine ya Mkoa Dar es salaam,Morogoro na Arusha.

Katika shitaka la pili watuhumiwa hao wandaiwa Kutoa fedha kwaajili ya kufanya vitendo vya ugaidi;Mbowe anadaiwa kutoa fedha kwa Halfani Bwire,Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Abdilah Lingwenya kwa ajili ya kutekeleza vitendo vya ugaidi.

Kosa la tatu linawakabili watuhumiwa Halfani Bwire Hassan,Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Abdilah Lingwenya ambao wanashitakiwa kwa kujipatia fedha kutoka kwa Freeman Mbowe ili waweze kutekelez vitendo vya ugaidi kinyume cha sheria ya kuzuia ugaidi ya mwaka 2001.

Aidha washitakiwa wanakabiliwa na shitaka la kumiliki silaha kinyume cha sheria:Katika shitaka hilo Adam Kusekwa akiwa katika wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro anadaiwa kumiliki silaha aina ya pistol bila kuwa na leseni ya umiliki.

Katika shitaka jingine watuhumiwa wanadaiwa kumiliki risasi kinyume cha sheria:shitaka ambalo linamkabili Adam Hassan Kasekwa.

Aidha katika shitaka la tano linamkabili,Halfan Bwire Hassan ambaye anadaiwa kumiliki sare za jeshi kinyume cha sheria usalama wa Taifa.