March 23, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

HATUJATAKA FEDHA ZA AZAKI KUJA HAZINA- WAZIRI DKT. NCHEMBA

Na: Anthony Rwekaza

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa ufafanuzi kuwa Serikali haina nia ya kuchukua fedha zinazotolewa na wafadhili kwenda kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali (AZAKI), isipokuwa wao wanasisitiza kuwa AZAKI baada ya kupokea fedha hizo zijikite katika miradi ya maendeleo na malengo ya Serikali.

Akizungumza Machi 28, 2022 ambapo ametolea ufafanuzi madai ya kauli yake aliyoitoa hivi karibuni iliyoonekana kuibua utata, aliyoitoa akiwa Jijini Dodoma baada ya kikao chake kwa njia ya mtandao na Mkurugenzi wa USAID kuhusu ushirikiano baina ya shirika hilo  na Serikali ya Tanzania, ambapo alitoa wito au pendekezo kwamba msaada wa fedha takribani Trilioni 3 ambazo USAID imepanga kuipatia Tanzania kupitia Asasi za Kiraia (AZAKI), zielekezwe kwenye miradi ya kipaumbele ya Serikali.

Kauli hiyo ilichukua sura tofauti kwenye mitandao ya kijamii, magazeti hata kwenye vyombo vingine vya habari, baadhi ya wadau waliitafsiri kuwa Serikali inalenga kuchukua fedha hizo au kuwapangia walengwa namna ya kutumia, kufuatia utata huo Waziri huyo ametolea ufafanuzi kuwa yeye alichokifanya ni kuwaeleza washirika wa maendeleo kuhusu mifumo ya Bajeti ya Serikali, ambapo amebainisha kuwa Serikali haina nia ya kuchukua fedha zinazokwenda kwa AZAKI hisipokuwa ufadhili huo uende sambamba na malengo ya Serikali

“Kama Waziri mwenye dhamana ya Fedha nina Wajibu wa kuwaeleza washirika wa Maendeleo kuhusu mifumo yetu ya Bajeti. Ndicho nilifanya katika mazungumzo na USAID . Hatuna nia ya kuchukua fedha zunazokwenda AZAKI, isipokuwa ufadhili uendane na malengo yetu” amesema Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba

Pia Waziri huyo kuwa hakumanisha kuwa USAID wachukue Fedha walizotaka kuwapa AZAKI na kuipatia Serikali, bali USAID wanaotoa fedha na AZAKI zinazopokea fedha wanatakiwa waelekeze nguvu zao katika miradi inayoendana sanjari na Dira ya Taifa, pamoja na mipango na vipaumbele vya Serikali.

Ameongeza kuwa fedha ambazo utolewa na washirika kwa ajili ya maendeleo uzipeleka moja kwa moja kwa AZAKI, ambazo amedai kuwa fedha hizo usimamiwa na menejimenti au Bodi ya AZAKI kwa mujibu wa sheria ya NGO, amesema kuwa fedha zinazotumiwa na Serikali zinatakiwa kufuata matakwa ya Bajeti na Sheria ya Fedha za umma kama inavyolekeza kisheria. Amesisitiza kuwa hawajataka fedha za AZAKI kwenda HAZINA

“Fedha ambazo washirika wa Maendeleo wanazipeleka moja kwa moja kwa Azaki zinasimamiwa na menejimenti/Bodi za Azaki kwa mujibu wa Sheria ya NGO. Fedha zinazotumiwa na Serikali zinapaswa kufuata Sheria ya Bajeti na Sheria za Fedha za umma. Hatujataka Fedha za AZAKI Kwenda Hazina” amesema Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba

Hata hivyo amezitaka AZAKI kuwianisha shughuli zao na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Mpango wa Maendeleo wa Miaka tano ili kwa pamoja Serikali, sekta Binafsi na Jamii kupitia CSOs wavuke kwa pamoja katika kuleta Maendeleo ya Nchi ya Tanzania. Pia amewasihi DPs kuongeza Fedha kwa CSOs

Ufafanuzi huo umelenga kuleta majibu ya mjadala ambao ulikuwa gumzo kwa baadhi ya wadau hasa wanufaika wa fedha hizo NGO.