Na: Anthony Rwekaza
Hukumu ya Kesi ya Jinai Namba 105/2021 inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na wenzake wawili Sylvester Nyegu (26) na Daniel Mbura (38) imepangwa kutolewa Oktoba 1,2021 katika Mahakama ya Hakimu Makazi Arusha.
Akizungumza hayo Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo anayesikiliza kesi hiyo ya jinai ya unyanganyi wa kutumia silaha amefikia amesema ushahidi wa upande wa mashtaka na ule wa utetezi umefungwa kinachosubiriwa ni utaratibu wa uhukumu iliyopangwa kutolewa October Mosi, 2021.
Juni 4, 2021, Mshtakiwa Lengai Ole Sabaya alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa mara ya kwanza baada ya kushikiliwa na Idara ya Upelelezi ya Serikali ya Tanzania akihojiwa kwa tuhuma mbalimbali, kufuatia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan siku chache baada ya kuingia madarakani kumsimamisha Ukuu wa Wilaya ya Hai na kuelekeza mamlaka kumchunguza kufuatia uwepo madai ya tuhuma mbalimbali dhidi yake.

Baada kufikishwa Mahakamani alisomewa mashtka ya unyanganyi wa kutumia silaha, lakini Wakili wa Serikali Tumaini Kweka aliomba kuondoa shauri hilo Mahakamani kama ilivyoanishwa kwenye Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kifungu 9(1) iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019, Hakimu Odira Amwaro aliridhia ombi hilo kuondolewa na kufunguliwa upya licha ya mashtaka mengine yaliyokuwepo awali kufutwa.
Upande wa utetezi umetoa utetezi wake uliofungwa rasmi Augosti 24, 2021 ukiwakilishwa na Wakili Moses Muhuna, Dancon Oola, Edimund Ngemela, Sylvester Kahunduka, Fridolin Gwemelo na Jeston Justin huku kwa upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Tumaini Kweka, Abdallah Chavala, Felix Kwetuka na Baraka Mgaya chini ya Hakimu Odira Amworo aliyetolewa Mkoani Geita kuja kuendesha shauri hilo kufuatia taratibu za Mahakama.
Kwa sasa Lengai Ole Sabaya pamoja na wenzake wawili wanakabiliwa na shtaka la unyanganyi wa kutumia silaha wanalodaiwa kulitenda Feburuari 9, 2021 kwenye duka la Mfanyabiashara Mohamed Said maeneo ya bondeni Mkoani Arusha, watuhumiwa wamerudishwa Gereza la Kisongo kufuatia
makosa yanayowakabili kutokuwa na dhamana.
Habari Zaidi
DCI KINGAI ASISITIZA WAZAZI KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA UKATILI
THRDC,C-SEMA YAENDESHA MAFUNZO KWA POLISI NA WAENDESHA MASHITAKA