Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya leo Juni 28,imemuachia huru Mwanaharakati maarufu wa mitandaoni na mfuasi wa Chama Cha upinzani cha CHADEMA, Mdude Nyagali baada ya kukaa rumande kwa zaidi miezi 12.Mahakama imemuachia huru baada ya Jamhuri kushindwa kuthibitisha pasina shaka tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Mnamo Mei 13, 2020 mwanaharakati huyo alikamatwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya kwa tuhuma za Makosa mtandaoni.
Hata hivyo, alipofikishwa mahakamani alisomewa mashitaka ya uhujumu uchumi ambapo alidaiwa kukutwa na dawa za kulevya ya Heroini kiasi cha gramu 23.4 kinyume na Sheria Kudhibiti Dawa za Kulevya namba 5 ya mwaka 2015 iliyofanyiwa marekebisho,pamoja na aya ya 23 ya sura kwanza na kifungu namba 57 (1) na 60 (2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi pamoja Njama za Kupanga Uhalifu (Sura ya 200 tolea la mwaka 2002).
Hata hivyo tarehe 27 Mei 2020,Jamhuru iliiondoa kesi hiyo na kuifungua upya ikimshtaki Mdude kwa kusafirisha Dawa za Kulevya aina ya Heroini kinyume cha sheria ya Kudhibiti Dawa za kulevya.Alinyimwa dhamana mpaka leo Juni 28 alipoachiwa huru.
Habari Zaidi
GENGE LA VIJANA WA KISUKUMA KATAVI LAFUMWA LIKIFANYA “CHAGULAGA”.
AFRICAN COURT ON HUMAN AND PEOPLES’ RIGHTS DELIVERED 14 JUDGMENTS
KESI YA MBOWE:SHAHIDI WA TATU (JAMHURI) AANZA KUTOA USHAHIDI.