February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

HALI TETE NGORONGORO

Mnamo Mwaka 2019 kile kinachodaiwa kuwa ni uamuzi wa serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kipindi hicho Waziri akiwa Kigwangala ulisainiwa Mkataba wa kuhamishwa Budget ya Ngorongoro Pastoralist Council (NPC) kwenye Halmashauri ya Wilaya ya ngorongoro, Ikumbukwe kuwa NPC ni chombo kinachowakilisha au sauti ya jamii waishio Tarafa ya Ngorongoro ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Hivyo jamii haifurahii wala hainufaiki na haki za binadamu kama ilivyoingizwa kwenye katiba ya 1984, Kifungu cha sheria ya NCAA ya 1959 5 (A) imetaja kuwa NCAA wana jukumu la kuendeleza wenyeji.

Mkataba huo ulisainiwa mbele ya Waziri Kigwangala 2019, Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Technolojia Tate William Olenasha na kusainiwa na Mw/kiti wa NPC Ndg Maura kwa kile kinachodaiwa kuwa usimamizi mbovu/ ubadhilifu, hata hivyo waliohisiwa ni Viongozi wa NPC wakiongozwa na Mw/kiti Maura, Jamii ilitegemea kama hatua ingechukuliwa kwa wahisiwa na sio kuhamisha pesa.

Athari za Mkataba huo zimeshaonekana na Wananchi wanapitia wakati mgumu sana, ikumbukwe kuwa gawio la bajeti hiyo isiopungua Bil.1.6 kwa mwaka ambayo kimsingi NPC walikuwa wakipokea kutoka NCAA kwa mujibu wa sheria na ilikuwa ikitumika katika maendeleo kadha wa kadha ndani ya jamii (Tarafa) ikiwepo Swala la Elimu.

Tangu kusainiwa kwa Mkataba huo wa kuhamisha Pesa Halmashauri, Swala la Elimu limekuwa hafifu, Chombo kile kimekuwa mfu haina sauti tena, haina majukumu tena, Kwani shughuli zote na matumizi ya bajeti imekuwa ikiratibiwa na NDC na kufanya ucheleweshaji wa shughuli za maendeleo ndani ya Tarafa haswa swala la Elimu, Wanafunzi hawaendi shule kwa wakati, Wanafunzi wengi wameacha kuendelea na shule kutokana na huduma yao kuchelewa hivyo kushindwa hata kufanya mtihani.

Wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro wamepokonywa na kudhulumiwa Haki yao ya msingi.