February 3, 2023

Watetezi Media

Official Website for Watetezi Media

HALI BADO TETE GAZA,VIFO VYAFIKIA 219

Na Leonard Mapuli.

Ndege za kivita za Urusi zimeendelea kutanda katika anga la Palestina zikishambulia nyumba za makazi ya watu ambapo kwa leo pekee (May 19) watu wanne wameuawa akiwemo mwandishi wa Habari nchini Palestina.

Israel imeongeza mashambulizi zaidi baada ya Palestina  kushambulia kwa maroketi majiji yaliyoko Kusini mwa Israel ambayo hata hivyo hakuna taarifa za vifo wala majeruhi.

Duru zinaarifu kuwa mapema Jumatano hii,vikosi vya Israel pia viliwaua Wapalestina wanne na kujeruhi kadhaa waliokuwa wakiandamana  ambayo yanatajwa kuwa ya kihistoria eneo la West Bank na Mashariki mwa mji mtakatifu wa Jerusalem.

Mapigano kati ya Israel  na Palestina yameingia siku ya nne ambapo mbinu zakidiplomasia  kumshawishi Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyau na kiongozi wa kikundi cha Hamas kinachoukalia mji wa Gaza zimegonga mwamba.

Marekani bado imeshikilia msimamo wake kutokuliunga mkono baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa  katika waraka wa pamoja kutaka pande hizo mbili kusitisha mapigano hayo yaliua watu 219 hadi sasa.

Bunge la Muungano wan chi za kiarabu limefanya kikao chake isivyo kawaida na kuishutumu zaidi Israel kuishambulia Palestina na kuua watu wasio na hatia ambapo bunge hilo linadhamiria kuishtaki Israel kwa uhalifu wa kivita  na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Maafisa wa afya wa Palestina  wameonesha wasiwasi wa wimbi jipya la kusambaa kwa virusi vya Corona baada ya maabara iliyokuwa ikitumiwa kushindwa kufanya kazi baada ya kuharibiwa na bomu la anga lililopigwa na vikosi vya Israel kwenye jengo lililo jirani na maabara hiyo.